Je kuna sheria gani za binadamu kutumia eneo fulani la sakafu ya mwezi na kudai umiliki?

Buzz Aldrin, 1969

Chanzo cha picha, NASA

Maelezo ya picha, Buzz Aldrin was taken by the Moon's emptiness

Kampuni na mataifa kadhaa yameanza kutafuta njia za kuchimba madini ya thamani kaika sakafu ya mwezi.

Je kuna sheria gani za binadamu kutumia eneo fulani la sakafu ya mwezi na kudai umiliki?

Ni takriban miaka 50 tangu Neil Armstrong kuwa mtu wa kwanza kutembea mwezini.

Hiyo ni hatua moja ndogo kwa binadamu, mwanaanga huyo wa Marekani alisikika akisema mara kwa mara huku akiongezea kuwa ni hatua kubwa iliopigwa na wanadamu.

Muda mfupi baadaye , mwenzake Buzz Aldrin aliungana naye .

Baada ya kushuka katika chombo hicho, alitazama sakafu hiyo iliokuwa bila chochote juu yake na kusema: Uharibifu mkubwa.

Tangu ujumbe wa Apollo II mnamo mwezi Julai 1969, mwezi haujaguswa.-hakuna binadamu mwengine yeyote aliyekwenda mwezini tangu 1972.

Lakini hilo huenda likabadiliki hivi karibuni huku kampuni kadhaa zikiwa na hamu ya kuchunguza na kuchimba madini yenye thamani ikiwemo dhahabu, platinum na madini mengine yasiopatikana duniani ambayo hutumika katika vifaa vya kielektroniki.

Mapema mwezi huu, China ilipeleka chombo Chang'e-4, katika eneo la mbali la mwezini na ikafanikiwa kuotesha mbegu ya pamba katika sakafu yake.

Pia Inapanga kuanzisha makao ya utafiti.

Kampuni ya angani ya Japan iSpace inapanga kujenga kifaa kinachoweza kusafirisha vitu kutoka mwezini hadi duniani huku ikichunguza maji yaliopo mwezini.

Uwezekano wa umiliki wa sayari umekuwa swala muhimu tangu uchunguzi wa angani ulipoanzishwa wakati wa vita baridi..

Huku Nasa ikipanga kupeleka ujumbe wake angani , Umoja wa mataifa pamoja na azimio la angani ikiwemo mwezini na viumbe vyengine vya angani havimilikiki kwa matumizi ama kwa njia nyengine zozote.

Kuna mpango miongoni mwa baadhi ya kampuni kuanza kuchimba madini ya thamani mwezini.

Joanne Wheeler, mkurugenzi wa kampunni ya angani ya Alden Advisers, ameelezea maamuzi hayo kama "the Magna Carta of space".

Inapanga kuweka bendera mwezini kama vile ambavyo Armstrong na warithi wake walivyofanya.

Kwa uhakika, umiliki wa ardhi na haki ya uchimbaji mwezini haukuwa muhimu sana mwaka 1969.

Lakini huku teknolojia ikimaarika, uchimbaji wa mali hiyo asli ili kujipatia faida limekuwa swala muhimu la siku zijazo.

Mwaka 1979, Umoja wa mataifa ulitoa makubaliano yanayosimamia vitendo vya mataifa mwezini pamoja na sayari nyengine yanayojulikana sana kuwa makubaliano ya mwezini.

Makubaliano hayo yanasema kuwa mwezi unafaa kutumiwa kwa njia za amani.

Na umoja wa mataifa ni sharti uelezewe ni wapi na kwa nini mtu anataka kuweka kituo mwezini.

Makubaliano hayo pia yanasema kuwa '' Mwezi na mali asli zake ni urithi wa mwanadamu na kwamba utawala wa kimataifa unafaa kubuniwa kutawala uchimbaji wa mali hiyo iwapo itawezekana.

Tatizo la makubaliano hayo ya mwezini , hatahivyo ni kwamba ni mataifa 11 pekee ambayo yametia saini.

Ufaransa ni mojwapo na India ni taifa jingine. Mataifa yenye uwezo mkubwa ikiwemo China, Marekani , Uingereza na Urusi hazijatia saini makubaliano hayo.

Bi Wheeler anasema kuwa sio rahisi kushinikiza kufuatwa kwa makubaliano hayo .

Mataifa tofauti yanaheshimu sheria hiyo na yana kazi ya kuhakikisha kuwa makampuni na watu binafsi pia wanaheshimu.

Cheti cha kumiliki ardhi mwezini 1955

Chanzo cha picha, Getty Images

Profesa Joanne Irene Gabrynowicz, muhariri wa zamani wa jarida la angani la Space Law, anakubaliana kwamba makubaliano ya kimataifa hayatoi hakikisho.

''Makubaliano hayo ni swala gumu linaloshirikisha siasa, uchumi na maoni ya raia'', aliongezea.

Na maamuzi yaliopo ambayo yanapinga mataifa kumiliki sayari yanakabiliwa na changamoto zaidi katika siku za hivi karibuni.

Mwaka 2015, Marekani ilipitisha sheria ya kutumia anga kufanya biashara, ambayo inawapatia raia wake haki ya kumiliki mali yoyote asli ambayo wataweza kuchimba katika sayari.

Hatahivyo sheria hiyo haishirikishi uchimbaji wa mali asli mwezini lakini sera hiyo inaweza kupanuliwa na kushirikisha mwezi

Mwezi mkubwa kama ulivyoonekana kutoka Itali.

Chanzo cha picha, Getty Images