Urusi barani Afrika: Je inakuwa kiungo muhimu?

Army officers at Moscow defence show

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Maafisa wa jeshi la nje wanakagua zana katika maonyesho ya ulinzi Urusi

Shughuli za hivi karibuni za Urusi nchini Sudan na Afrika ya kati zimezusha uvumi mwingi.

Hiyo ni kutokana na kuwa kando na kufufuliwa kwa uhusiano wa kiuchumi, wakandarasi wa kibinafsi wa Urusi wanaripotiwa kujishughulisha katika nchi zote mbili.

Hili ni zaidi kwa nchi ya Sudan ambako kumeshuhudiwa maandamano dhidi ya serikali yaliosambaa na kwa mara nyingi yanayokumbwa na ghasia.

Moscow imeonekana mara kwa mara kuigeukia Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, kuendeleza uchumi, usalama na ushirikiano wa kiulinzi.

Kwa hivyo, tunafanya nini kuhusu shughuli za Urusi barani Afrika, na ni shughuli kubwa kiasi gani?

President Putin and Basir

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Putin na Basir

Mamluki wa Urusi?

Kwa wiki nyingi sasa, watu nchini Sudan wameandamana katika mioji tofuati nchini, wakiishutumu serikali kwa kusimamaia vibaya uchumi wa taifa hilo.

Huku kukishuhudiwa wasiwasi huo, kumekuwa na shutuma kutoka kwa baadhi ya waandamanaji na katika vyombo vya habari kwamba wakandarasi wa Urusi wamekuwa wakisaidia au kushauri vikosi vya usalama Sudan.

Uchunguzi wa idhaa ya Kirusi ya BBC mwaka jana umesikia ushahidi kutoka duru waliokaribu na maafisa wa ulinzi kwamba mamluki kadhaa wamekwenda Sudan.

Katika nchi jirani Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR), Moscow imekuwa ikishinikiza uhusiano wake wa kiusalama na serikali inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa.

Lakini uvumi kuhusu kiwango cha shughuli za Urusi huko CAR uliongezeka mwaka jana Julai baada ya vifo vya waandishi watatu wa Urusi , waliokwenda kufanya uchunguzi wa taarifa za kuwepo Mamluki nchini humo.

maafisa wa Urusi hivi karibuni wamepuuzilia mbali ripoti za uwepo mkubwa wa mamluki katika CAR.

Lakini baadhi ya wachambuzi wanaamini vikosi vya jeshi vya kibinafsi vina umuhimu - iwapo havijatangazwa - katika maenoe ambako Urusi inatafuta kuendeleza au kupanua ushawishi wake.

Na katika mkutano na waandishi habari mnamo Desemba, Rais Vladimir Putin aliulizwa kuhusu kundi la mamluki na akasema wana haki "ya kuendeleza azma zao kibiashara kokote katika sayari".

Soviet military parade

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Je Urusi inarudi katika nyakati za Sovieti?

Kurudi Afrika

Uliyokuwa Muungano wa Sovieti ulikuwa mshirika muhimu katika bara la Afrika - hadi ushawishi wake kiuchumi na kisiasa ulipofifia kwa kumalizika kwa vita vya baridi.

Leo, Urusi, "inatafuta kuirudisha na kuimarisha nafasi yake katika bara la Afrika", kwa mujibu wa Inna Andronova, kutoka chuo cha Higher School of Economics mjini Moscow.

Njia moja ni kupitia usafirishaji wa silaha zake nje.

Licha ya kwamba baadhi ya masoko yake yako Asia, mauzo yake kwa Afrika ni muhimu na yanakuwa.

USAFIRISHAJI WA SILAHA ZA URUSI

Mteja wake mkuu kartika bara hili ni Algeria, kwa mujibu wa data zilizotolewa na taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani - Stockholm International Peace Research Institute (SIPRI).

Msiri, ambayo kwa miaka mingi imekuwe ikipokewa msaada wa kijeshi kutoka Marekani imeanza kuwa mteja muhimu kwa Urusi pia.

Lakini data za SIPRI kuhusu usafirishaji wa silaha kubwa unaonyesha pia kwamba kati ya 2016-17, Urusi ilipokea received orders from or made deliveries to a range of other African countries:

  • Angola
  • Burkina Faso
  • Cameroon
  • Guinea ya Ikweta
  • Ghana
  • Mali
  • Nigeria
  • Sudan Kusini
  • Sudan

Zilijumuisha helikopta za usafiri na za kivita, ndege za vita na makombora ya ulinzi, na kwa mara nyingi i ambazo zimetumika, au kuukuu ambazo zimekarabatiwa upya.

Vifaa vya kijeshi vya Urusi huwa sio ghali mno ikilinganishwa na za mataifa ya magharibi na bado huwa madhubuti, jambo linaloyavutia mataifa maskini.

Vivutio vya utajiri wa rasilmali

Ni wazi Urusi ina malipo mazuri kiuchumi kwa kujihusisha katika bara la Afrika.

Ina uhaba wa madini kama vile manganese, bauxite na chromium, zote ambazo ni muhimu kwa viwanda.

Diamond mine

Chanzo cha picha, Petra Diamonds

Maelezo ya picha, Uchimbaji wa madini ya Almasi unaivutia sana Urusi

Kampuni ya Aluminium, Rusal, imenaz akusafirisha bauxite kutoka machimbo nchini Guinea, amabyo kwa sasa inakadiriwa kugharamia robo ya uzalishaji wa mtapo wa kampuni hiyo .

Urusi inavutiwa pia na Almasi - kampuni ya kitaifa ya uchimbaji madini, Alrosa, ilitia saini mkataba na Angola mnamo 2017.

Katika mwaka uliopita Urusi imetia saini mikataba kushinikiza uchumi na Angola, Namibia, Msumbiji, Zimbabwe na Ethiopia.

Iliidhinisha mkataba pia mnamo Agosti 2018 kuidhinisha kituo cha biashara katika bandari nchini Eritrea.

Lakini katika mtazamao wa kimataifa, BIashara ya Urusi barani Afrika imedididmizwa na uhusiano wa kibiashara wa taifa hilo na Ulaya, Asia na Marekani.

WASHIRIKI WA BIASHARA URUSI

Washindani wa Urusi

Ni muhimu kukumbuka kwamba mataifa mengine yanayoinukia kiuchumi kama China, India na Indonesia yamepanua kwa ukubwa biashara na Afrika katika miaka ya hivi karibuni.

Licha ya hayo huenda Urusi inaona nafasi kurudisha nafasi yake kimataifa kwa kushinikiza ushirikiano na Afrika.

Urusi imempokea mara kadhaa rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye anakabiliwa na mashatka katika mahakama ya kimataifa ya jinai kwa uhalifu wa kivita.

Lakini kuna mipaka kwa yale ambayo Urusi inaweza kuyafikia, baadhi ya wachambuzi wanaamini.

Alex Vines, wa Chatham House, anaashiria kuwa Urusi sio uliokuwa muungano wa Sovieti.

"Haina rasilimali kujipanua kwa ukubwa Afrika. Badala yake itatafuta nafasi kama vile katika ulinzi na utafutaji wa mali ghafi," anasema.

Hatahivyo, sio vigumu kutambua hamu mpya ya Urusi.

Ikitangaza mpango mpya kwa Afrika mwaka jana Desemba, Marekani ilishutumu kuongezeka kwa shughuli za Urusi na China katika bara hili.

Imesema Urusi, inaendeleza uchumi na siasa zake pasi kuzingatia sheria, na utawala wa uwazi na uwajibikaji.