Wabunge 300 waidhinisha mswada wa mageuzi ya katiba

Chanzo cha picha, AFP
Wabunge nchini Sudan wameunga mkono mpango wa kubadilisha katiba ya kumkubali Rais Omar-al-Bashir kuwania kwa muhula wa tatu mwaka wa 2020.
katiba ya nchi hiyo ilibadilishwa mwaka 2015 na kufanya Ma rais kuwania mihula miwili pekee.
Iwapo katiba haitabadilishwa basi Rais Bashir atalazimika kuondoka madarakani.
Bashir alichukua uongozi wa taifa hilo kwenye mapinduzi ya kijeshi miaka thelathini iliyopita.
Spika wa bunge amesema kuwa takriban wabunge mia tatu wamesaini azimio la kuunga mkono mswada huo wa mageuzi ya katiba.
Katiba hiyo ikipitishwa basi Rais Bashir mbali na kupata muhula wa tatu, atakua na mamlaka ya kuwafukuza magavana .

Chanzo cha picha, Reuters
Mwaka 2016 Bashir aliiambia BBC kuwa ataachia madaraka mwaka 2020. Alisema kuwa kazi yake inachosha na huu ndio muhula wake wa mwisho.
Ameingia madarakani mwaka 1989, na alishinda uchaguzi wa mwisho wa urais nchini Sudan, alishinda Kwa asilimia 94 ya kura na kuwaacha mbali wapinzani waliolalamika kuwa uchaguzi haukua wa haki.
Bashiri alikanusha madai ya ICC ya kuhusika na uhalifu wa kivita na kusema kuwa ni njama za kisiasa , na ushahidi alionayo ni kiasi gani anapendwa na watu wa Sudan, hivyo angekua amefanya uhalifu wasingekua wakimpokea vizuri.
Wakosoaji wa Bashir wanasema kuwa akiingia muhula wa tatu, hali ya uchumi itakua mbaya Zaidi kutokana na vikwazo kuongezeka.
Sudan iliwekewa vikwazo vya kibiashara na Marekani baada ya baadhi wa wapiganaji wa kiislam kuingia Sudan. Osama Bin Laden aliingia na kukaa Sudan miaka ya 90,
Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Sudan kusini kujitenga na kumiliki Zaidi ya aslimia 70 ya vyanzo vya mafuta, na kupunguza mapato makubwa Sudan.

Chanzo cha picha, Reuters
Mbali na kuwekewa hati ya kimataifa ya kukamatwa na mahakama ya kivita ya ICC, alipigwa marafuku pia kusafiri, lakini Bashir ametengeza uhusiano wa Kidiplomasia na kutembea Misri, Saud Arabia na Afrika kusini.
Mbali na kuwa Rais huyu wa Sudan alikua akisisitiza juu ya Umoja wa Sudan, mwaka 2011 Sudan kusini ilijitenga kwa kura asilimia 99 kutoka kwa watu wa Sudan Kusini.
Omar al-Bashir ni nani?
- Alipigana vita ya jeshi la misri na vita ya Waarabu na Israel.
- Aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi mwaka 1989
- Alimpatia hifadhi kiongozi wa Al-Qaeda Osama Bin Laden miaka ya 1990.
- Rais wa kwanza kushatkiwa na ICC.
- Ameshutumiwa na uhalifu wa kivita Darfur lakini alikana.
- Alisaini makubiliano ya amani na wapiganaji wa kusini 2005.













