Dereva wa Uber akiri kuua watu sita nchini Marekani

Chanzo cha picha, Reuters
Dereva wa Uber anayeshutumiwa kufanya mauaji ya watu sita kwa nyakati tofauti katika jimbo la Michigan nchini Marekani mwaka 2016 amekiri makosa ya kuuwa, kutaka kuuwa na matumizi mabaya ya silaha.
Watu wanne waliuawa katika mgahawa, na wawili katika gereji ya magari wakati wa maigano ya risasi mjini Kalamazoo.
Jason Dalton mwenye umri wa miaka 48, awali alielekeza shutuma zake kwa programu ya simu ya Uber kuwa inadhibiti akili na mwili wake.
Lakini alibadili kauli yake muda mchache kabla ya kusikilizwa tena kwa kesi yake.
Hakuna chochote alichoahidiwa bwana Dalton ili akiri kuuwa, wakili alisema.
Mashtaka yake yamejumuisha makosa matatu, kutaka kuua mara mbili, kuuwa watu sita na matumizi mabaya ya silaha. Na sasa anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha.
Bwana Dalton ambaye aliwasilisha mpmajibu yake ya kukiri kuuwa wakati wa kikao cha jopo la majaji, alifanya hivyo japokuwa alizuiwa na mwanasheria wake.
Alimwambia hakimu wa mahakama ya jimbo la Kalamazoo kuwa alifanya maamuzi kwa hiari yake, akiongeza kuwa alitaka kufanya hivya kipindi kirefu kilicho pita.
Awali inasemekana kuwa Dalton aliwaambia polisi kuwa alifanywa kuwa kibaraka na programu ya simu ya Uber ambayo ilimwongoza kupiga watu risasi watu tofauti kwa zaidi ya saa tano mwezi Februari 2016.
Japokuwa waliouwawa hawakuwa wateja wa Uber, polisi wanasema Dalton aliendelea kupakia wateja wakati wa masaa ya kupiga watu risasi jimboni Kalamazoo, mji mdogo uliopo mile 150 magharibi mwa Detroit.
Mauaji hayo yalifanyika siku ya jumamosi jioni katika maeneo matatu tofauti nje ya mgahawa wa Cracker Barrel, duka la magari ya Kia na katika gorofa moja yenye nyumba za kupangisha.
- Mapigano ya awali ya risasi yalifanyika katika jengo la kalamazoo. Mwanamke alipigwa risasi kadhaa majira ya 17;00 inasemekana mbele ya watoto wake alipelekwa hospitali kwasababu alikuwa na hali mbaya.
- Majira ya saa 22:00 saa za Marekani, baba na mtoto walipigwa risasi na kuuawa na mtu wa tatu alipata majerana katika duka la magari.
- Majira ya saa 22:15, mapigano ya tatu ya Risasi yalifanyika katika sehemu ya kupaki magari kwenye mgahawa wa Cracker Barrel ambapo Mary Lou Nye mwanamke wa miaka 62 aliuawa, akiwepo Doroth Brown 74, Barbara Hathorne 68 na Mary Jo Nye 60 huku binti wa miaka 14 akinusurika kuuawa.
Baada ya kukamatwa na polisi, kampuni ya Uber ili thibitisha kuwa Dalton ni dereva aliyesajiliwa na kampuni hiyo ya usafiri, huku wakitoa taarifa rasmi kuwa tukio hilo ni lakutisha na lina vunja miayo.
Dalton alipelelezwa maisha yake kipindi cha nyuma lakini alifaulu kwasababu hajawahi kuwa na rekodi yoyote ya uhalifu.












