Mshukiwa wa shambulio la ugaidi la Strasbourg Ufaransa atajwa ni Chérif Chekatt

Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi nchini Ufaransa wanamtafuta Chérif Chekatt, anayedaiwa kutekeleza shambulio la kigaidi lililofanyika hapo jana karibu na soko moja maarufu mjini Strasbourg.Polisi wa Ufaransa wakishirikiana na wale wa Ujerumani wanaendelea na jitihada za kutaka kumnasa.
Polisi wamesema kuwa Chérif Chekatt, mwenye umri wa miaka 29 nndiye wanamhusisha na shambulio hilo ,tayari alikuwa akifuatiliwa nyendo zake na mamlaka za usalama nchini Ufaransa tangu alipokuwa kifungoni baada ya kubainika na kosa la unyang'anyi na baadaye akajiunga moja ya kundi la ugaidi.
Watu 12 walikuwa wameumia na wengine sita waliumia vibaya.
Chérif Chekatt ni jina ambalo lilitajwa na mwandishi mmoja wa nchini humo na kudai kuwa alijulikana na vyombo vya ulinzi na anasakwa na polisi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 aliyejeruhiwa na risasi pamoja na kisu aliweza kutoroka eneo la tukio kwa kutumia gari ndogo ya kukodi, Heitz alisema.
Mshambuliaji huyo alimuamuru dereva ambaye alizungumza na polisi kuwa aliwauwa watu 12 na mtuhumiwa huyo ambaye amekimbia amekuwa akitafutwa na polisi kwa tuhuma za ujambazi.
Watu wengine wanne walishikiriwa na polisi usiku mzima kwa kuzaniwa kuwa walihusika na shambulio hilo.
Mamia ya maafisa walihusika katika msako wa muuaji huyo.Mapema naibu waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa , Laurent Nuñezalisema inawezekana kuwa mtu huyo hayupo tena nchini humo.
Waziri wa mambo ya ndani Christophe Castaner alisema hali hiyo inadhihirisha kiwango cha juu cha hatari.

Na kuongeza kuwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo ya mpaka katika masoko yote ya krismasi.
Meya wa Strasbourg, alisema maduka yote yatafungwa siku ya jumatano na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika maduka ya eneo hilo.
Shambulio hilo lilitokea majira ya saa mbili ya saa za Ufaransa siku ya jumanne katika eneo karibu na duka maarufu linalouza bidhaa za krismasi ambalo linawavutia watalii wengi katika msimu huu wa sikukuu.












