Ndege ya Merkel ilitua ghafla kufuatia hitilafu ya kiufundi

Chanzo cha picha, EPA
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atakosa ufunguzi wa mkutano wa G20 nchini baada ya ndege yake kulazimika kutua muda mfupi baada ya kuondoka Berlin.
Maafisa wa Bi Merkel na wajumbe wengine waliyokuwa wameabiri ndege hiyo wako walitua salama mjini Cologne kutokana na matatizo ya kimitambo.
Ndege hiyo iligeuzwa mkonda ilipokuw ajuu la anga ya Uholanzi, ilimesema shirika la habari la Ujerumani dpa.
Habari zaidi zinasema Merkel atasafiri mjini Buenos Aires leo( Ijumaa).
Hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusiana na tatizo la kiufundi iliyokumba ndege hiyo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, rubani aliwatangazia abiria kuwa ameamua kugeuza mkondo wa safari na kurudi alikotoka kufuatia kile alichosema kuwa "hitilafu ya mifumo kadhaa ya kielektroniki.''

Chanzo cha picha, EPA
Ndege hiyo aina ya Konrad Adenauer ililakiwa uwanjani na magari ya kutoa misaada.
Ripoti zinasema Bi Merkel na ujumbe wa Ujerumani baadae walisafiri kwa basi hadi hoteli moja mjini Bonn.
Vyombo vya habari vya Ujerumani vimeongeza kuwa Kansela Merkel na waziri wake wa fedha, Olaf Scholz, wanatarajiwa kusafiri nchini Argentina baadae leo (Ijumaa).
Ni mara ya kwanza ndege hiyo aina ya Aiabus A340 iliyopewa jina Konrad Adenauer kukumbwa na hitila ya kimitambo.

Chanzo cha picha, AFP
Huku hayo yakijiri Rais wa Marekani Donald Trump amefutilia mbali mkutano uliyokuwa umepangwa kati yake na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kufuatia mzozo wa majini kati ya nchi hiyo na Ukraine .
Siku ya Jumapili meli za kivita za Berdyansk na Nikopol, pamoja na meli ya kuzisindikiza Yana Kapa, zilijaribu kusafiri mji wa bandarini kwenye Bahari Nyeusi wa Odessa kuelekea Mariupol katika Bahari ya Azov.
Ukraine inasema Urusi ilijaribu kuzizuia meli hizo zisiendelee na safari yake, ambapo meli moja iliigonga meli ya Yana Kapa.
Meli hizo ziliendelea na safari kuelekea mlango wa bahari wa Kerch, lakini zikapata njia imezibwa na meli moja kubwa.
Urusi wakati huo ilikuwa imetuma ndege mbili za kivita na helikopta mbili ambazo zilikuwa zikipaa angani katika eneo hilo na kufuatilia mwenendo wa meli hizo.
Siku ya Jumatano Trump aliiambia gazeti la Washington Post kuwa anasubiri "ripoti kamili" kuhusiana na mzozo huo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameilaumu Urusi kwa kusababisha mzozo huo.
Amesema atajadiliana na Rais Putin juu ya suaala hilo pembezoni mwa mkutano wa siku mbili wa G20 utakaofanyika nchini Argentina












