Ni jambo gani tunajifunza kutoka kwenye taarifa zisizo sahihi?

Chanzo cha picha, AFP
Watu huwa wana hisia tofauti tofauti ikija kwenye kusambaza habari, Uchunguzi wa kina uliofanywa na mradi wa BBC kuhusu habari zisizo sahihi 'FAKE NEWS' umegundua hilo.
Kuenea kwa habari zisizo sahihi kunaweza kuathiri taarifa za uhakika kuonekana za uongo na kutokuaminiwa.
Uchunguzi kuhusu taarifa zisizo sahihi katika mitandao ya kijamii kama Whatsapp na Facebook, imechunguza watu kutoka Nigeria, Kenya na India na kubaini kwamba watu huwa wanavutiwa na taarifa hizo za uongo ambazo zinawapa hofu na matokeo yake wanayafahamu lakini bado wanaendelea kuzifuatilia.
Utafiti huo unatusaidia kuelewa uhusiano kati ya taarifa sahihi na siasa za kawaida ambazo zinaenea katika mitandao ya kijamii.
Kwa nini taarifa zisizo sahihi ni jambo la kuzingatiwa?
- Kwa sababu zinaondoa uaminifu
- Zinaleta mgawanyiko katika jamii
- Zinatishia dhana ya ukweli
- Ni hatari kwa vyombo vya habari- Vyombo vyote vya habari vinaweza kupata taarifa inayofanana na huku sio sahihi
- Taarifa hizi zinawafanya watu wapunguze uwezo wao wa kufanya maamuzi kulingana na ukweli
- Zinawaathiri wananchi katika kutoa taarifa
- Zinatishia afya za watu
- Zinatoa taarifa ambazo zinaweza kueneza chuki na kupelekea kuwepo kwa vurugu na vifo
- Zinavuruga harakati za kidemokrasia
- Zinatoa taarifa juu ya silaha
Kwa nini watu wanadanganyika na taarifa zisizo sahihi?
Watu wengi wana uelewa wa kutambua taarifa hizo zisizo sahihi, Uchunguzi wa BBC umebaini hayo ilipozungumza na watumiaji wa mitandao ya kijamii wa nchini Nigeria na Kenya.
Licha ya kuwa watu wengi wanaelewa matokeo ya kusambaza taarifa ambazo sio sahihi, na mara nyingi hali hii inaondoa kiwango cha dhana ya kweli.
Watafiti wamebaini kuwa uhusiano kuhusu taarifa zisizo sahihi na vitu kama vya vifaa vya umeme na masuala ya kidemokrasia huwa yanapendwa sana na watu.
Hisia binafsi huwa ndio sababu za usambazaji wa taarifa hizo, Watafiti hao walibaini. "Mara baada ya kuangalia taarifa hiyo niliguswa hivyo ilinipelekea kuwashirikisha wengine", mtu mmoja kutoka Nigeria alieleza.
Nigeria na Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zina uweleo mdogo wa teknolojia ya mitandao haswa katika maeneo ya vijijini ambapo taarifa yeyote iliyoandikwa katika mtandao wa Facebook kuonekana kuwa ya kweli, watafiti walieleza

Lakini Nigeria na Kenya wana afadhali kuliko India ikija kwenye suala la kuhakiki kama taarifa ni ya kweli au la.
Huwa wanahakiki kupitia mtandao wa Google pamoja na mitandao mingine.
Baadhi ya taarifa zisizo sahihi ni ngumu kuzingundua kuliko nyingine.
Wakati watumiaji wa mitandao wanapoonekana kuwa na kiwango sahihi cha kufuatilia taarifa za kisiasa nchini Nigeria , huwa ni vigumu kubaini kama taarifa hiyo ni sahihi ikiwa taarifa hiyo haitoki katika nchi husika, kwa mfano nchini Kenya, tarifa inayohusiana na siasa za kimataifa kama za utajiri wa mafuta Nigeria huwa ni vigumu kutambua ukweli wake.
Lakini vijana wengi hawazingatii kwenye maadili na shutuma za kidini kuliko vizazi vya kabla yao, na hii inapelekea kupugua kwa taarifa hizi zisizo sahihi kuenea zaidi.
Mambo gani mengi huwa yanasambazwa na taarifa zisizo sahihi?
Mara nyingi huwa wanajali ni nani ametuma lakini sio chanzo cha habari. Wanaweza kuamini kuwa taarifa ni ya kweli kama aliyetuma ni mtu anayeaminika.
Taarifa inaposambazwa kwa watu huwa inaaminika kuwa ya kweli.
Mtu kuwa wa kwanza kuituma taarifa katika kundi la marafiki zake huwa inaonyesha kuwa anafahamu na hivyo kuwahamasisha watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Wakati mwingine watu huwa wanatuma habari kwa wengine kwa haraka bila kujua kama ina ukweli au hapana.
Kusoma huwa ni ngumu lakini kusambaza ni rahisi.
Watafiti wamebaini kuwa watu wengi huwa hawazingatii taarifa za kwenye mitandao kwa kina na watumiaji wengi huwa wanaangalia vichwa vya habari bila kusoma maelezo zaidi ya habari hiyo wenyewe.
Kwa baadhi imekuwa mazoea.
Wanaweza kusambaza taarifa kwa sababu tu wanataka kuwatahadharisha watu na kutuma taarifa mpya kwa wengine.
"Inawezekana kuna mtu hajui kuhusu jambo fulani hivyo nikituma taarifa hiyo itaweza kuzuia jambo hilo lisitokee kwa rafiki yangu" Watu kadhaa walieleza hayo walipohojiwa na BBC nchini Kenya.



Wasambazaji wengi wanaamini kuwa upatikanaji wa taarifa uko sawa na kila mtu anataka kuchukua sehemu yake.
Watu wengine wanaamua kusoma taarifa hizo kwa sababu huwa zinafurahisha.
Nitajuaje kuwa hiyo taarifa sio sahihi?
Kama hauna uhakika na taarifa ,angalia uhakika wa habari hiyo kupitia Africa Check .
Africa Check na tovuti nyinginezo inafanya kazi ya kuhakiki ukweli wa taarifa. Ingawa changamoto ipo kwenye ufanisi wa kasi ya kuhakiki taarifa za uongo.
Kumbuka kuwa maoni ambayo yanatolewa katika vyombo vya habari vya mitandao na Facebook hayawezi kuaminika kila wakati.
Kwa sababu mtandaoni ndio sehemu ambayo taarifa hizo zisizo sahihi huwa zinajadiliwa na kusambaa.
Taarifa za kugushi kuhusu fedha na ajira huwa zipo nyingi sana katika mtandao ya kijamii barani Afrika, mtafiti alieleza.
Jinsi mambo yalivyo,watumiaji wengi wa mitandao wanasema kuwa huwa wanaishia kutumia hisia zao kuhakikisha kuwa taarifa hizo ni za kweli au la na kama watazisikia katika vyanzo vingine vya habari.
"Huwa ninaangalia vichwa vya habari na kama inavutia sana basi najua hiyo habari sio ya kweli", Mary kutoka Kenya aliiambia BBC.
Nikiona kitu chochote katika blogu huwa nnakiangalia mara mbili kuwa taarifa imeandikwa katika na blogu gani na je kuangalia kwenye Google kama taarifa hiyo imeandikwa na zaidi ya chanzo kimoja cha habari", Chijioke kutoka Nigeria.
Lakini njia mbili haziwezi kubainisha ukweli wa jambo.
Watafiti walitumia mifano miwili kuonyesha taarifa sahihi na isiyo sahihi:
- Imeandikwa katika mtandao wa twitter kuwa haki za jumuiya ya mashoga , ambayo kiuhalisia haipo , imezuia kampeni za uchaguzi upande wa upinzani unaoongozwa na Atiku Abubakar na kuandikwa katika magazeti mtandaoni nchini Nigeria.
- Picha ya gari lililoanguka nchini Pakistan limechukuliwa na mtumiaji wa Facebook na kudaiwa ajali hiyo imetokea Nairobi.

Kuhakiki taarifa inaweza kumuwia mtu vigumu , kwa sababu Afrika ina uhaba wa habari za kuaminika na sahihi katika sekta nyingi.
Hii inamaanisha kuwa uwepo wa taarifa isiyo sahihi ni rahisi.
Utafiti umebaini nini katika taarifa zisizo sahihi?
Matarajio na hofu nyingi katika taifa mara nyingi hutokana na taarifa zisizo sahihi.
Nchini Nigeria, 19% ya watu hawana ajira, na taarifa za uongo za ajira ziko 6.2% zinasambazwa katika mtandao wa WhatsaApp.
Inakadiriwa kuwa 3% ya taarifa zisizo sahihi zinasambaa katika WhatsApp kuhusu ugaidi na jeshi, na kuwafanya Wanaijeria kuwa na hofu na matukio ya wanamgambo wa kiislamu na mambo mengine mengi.

Taarifa za uongo kuhusu fedha na teknolojia ni tatu ya nne ya taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa nchini Kenya kupitia WhatsApp .
Taarifa kuhusu dini ni 8%, watafiti walibaini.

Watumiaji wa Facebook mara nyingi wanashindwa kutofautisha kati ya taarifa isiyo sahihi na iliyo sahihi, Timu ya utafiti ya BBC imegundua hilo kupitia tangazo waliloweka katika mtandao wa Facebook.












