Mbwa: Mambo 10 muhimu kuhusu rafiki huyu mkubwa wa binadamu

Dog enjoying a car trip sticking its head outside the an open window, fur ruffled by the breeze

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mambo muhimu kuhusu rafiki huyu mkubwa wa binadamu

John Bradshaw ni mwanasayansi ambaye anayechunguza uhusiano kati ya binadamu na wanyama. Amekuwa akichunguza chanzo cha mnyama bora zaidi anayefugwa

Haya ni mambo makuu kuhusu mbwa.

1. Mbwa hakutokana na mbwa wa porini

A pair of husky dogs pulling a sledge

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Usidanganywe na muonekano

Mbwa walitokana na mbwa fulani wa porini ambao walitoweka kutoka porini maefu ya miaka iliyopita

Leo hii mbwa wa porini huko Marekani na Ulaya ni binamu wa mbali licha ya waoa kuwa na DNA inayokaribiana kwa asilamia 99.

2. Huwa wa ukubwa unaotofautiana kuliko wa wanyama wengine wanaonyonyesha

Dogs of various sizes close-up

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ona tofauti

Kwa sababu ya binadamu kuingilia kati kuna tofauti kubwa kati ya mbwa kuliko mnyama mwingine yeyote anayenyonyesha wa msituni au anyefugwa.

3. Wana "pua la pili"

Three dog snouts poking from under a blanket

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wana pua la pili

Hiki ni kiungo kinachofahamika kama vomeronasal kilicho kwenye nafasi kati ya pua la mbwa na sehemu ya juu ya mdomo

Wanasayansi bado hawafahamu kazi ya kiungo hiki ni ipi, lakini baada ya kuwachunguza wanyama wengine kama paka na hutumia kiungo hiki kunusa harua iliyoachwa na mbwa wengine.

4. Si kuwa mbwawamepoteza kabisauwezo wa kuona rangi

Image of a pair of colour blindness glasses - we see a forest, mostly yellow and green

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jaribu kuona mahala ulipo

Mbwa huona kijani kibichi, manjanona samawati ka mavile sisi huona, lakini macho yao hayawezi kuona rangi nyekundu ambayo mara nyingi huonekana kama rangi ya kijivu.

5. Mbwa 'hutabasamu'

Black and white dog, seemingly smiling

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwa hutabasamu?

Mbwa hutabasamu lakini si kwa sababu ya kama zetu .

Kulingana na mwanasayansi Dr John Bradshaw, mbwa anaweza kutabasamu kumshawiki mmilike wake kumunyesha mapenzi.

Kwa hivyo mbwa hawana furaha kila mara wanapotabasamu.

6. Mbwa wanaweza kuwa na matumaini

Little white dog with a birthday cake - turquoise background

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nina miaka saba sasa

Sawa na binadamu mbwa wanaweza nao kuwa na matumaini ya kupata kitu fulani.

Utafiti wa kisayansi iligunduliwa kuwa mbwa fulani huwa wanapenda kuchunguza kitu licha ya kutokuwa na uwezo wa kupata chakula. Hata hivyo mbwa wengine hawakuwa na motisha ya kufanya hivyo.

Inaweza kuonekana kuwa mbwa wengine huwa na matumaini wa kufanikiwa huku wengine huwa hawatarajii lolote.

7. Mbwa hawajutii

A Spaniel sits in a freshly dug out whole on a lawn

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ninajua niliacha mfupa hapa

Wamiliki wengine wa mbwa hutambua kile wanafikiri kuwa ni kujutia kwa mbwa lakini sayansi imeonyesha kuwa hilo hutokana na tabia ya mwenye mbwa.

Kujutia ni hali ngumu - mbwa huwa na hofu kuwa huenda akaadhibiwa bila kujua amefanya nini.

8.Hufanya urafiki sana na binadamu.

A dog sleeping with a toddler

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rafiki wa binadamu

Mara mwana mbwa anajufunza kuwa wanadamu ni marafiki, hisia zake humwambia kuwa ndio njia tu ya kuweza kuishi na hufanya urafiki wa karibu na binadamu.

Hii ndiyo sababu mbwa wengine hukumbwa na msongo wakati akiachwa peke yao na uhusi kuwa wametelekezwa.

9. Mbwa hufanya urafiki usio wa kawaida na binadamu...

Woman, man and dog sitting on a pier, looking over a lake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwa hufanya urafiki usio wa kawaida na binadamu...

Viumbe wengine wanaonyonyesha hupata hisia kama za mapenzi na furaha lakini sasa mbwa wanajulikana kwa kuwa na hisia maalum ambazo huja kulingana na tabia na binadamu.

Wamiliki wengine wa mbwa wanaamini kuwa mbwa wao huwapenda lakini wanasayansi wana ushahidi tabia ya binadamu ndiyo huchangia pia tabia ya mbwa.

10. Ikiwa mbwahakutani na binadamu anaweza kuwa mbwa wa mwitu

An Australian golden dingo resting in the shade of a tree

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwa aina ya Dingo alijitenga na binadamu miaka 4000 iliyopita

Ikiwa mbwa hawezi kukutana na binadamu hadi umri wa miezi mitatu, anaweza kugeuka na kuwa mbwa mwitu.

Mfano mkuu ni mbwa wa anayejulikana kama Australian Dingo, ambaye ni aina fulani wa mbwa wa kufugwa ambaye aligeuka na kuwa mbwa wa msituni miaka elfu nne iliyopita.