Prince William: Azuru Tanzania ili kupiga vita ujangili

Mwanamfalme William wa Uingereza ameanza ziara yake ya siku tatu nchini Tanzania ikiwa sehemu ya juhudi zake katika kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama pori.

Mwanamfalme huyo ambaye yuko kwenye kampeni dhidi ya ujangili wa wanyama pori kama tembo,viboko na wanyama wengine.

Mwanamfalme leo ameanza ziara yake katika bandari ya Dar es salaam na ataweza kutembelea mbuga ya wanyama ya Mkomazi na atatembelea chuo cha wanyama pori kilichopo kaskazini mwa Tanzania 'College of African Wildlife Management in Kilimanjaro'.












