Mkasa wa MV Nyerere Tanzania : Magufuli avunja bodi ya Sumatra na ile ya ushauri ya Tamesa

Rais Magufuli
Muda wa kusoma: Dakika 3

Rais John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini SUMATRA Mhandisi Dkt. John Ndungura .

Taarifa ya Ikulu iliotolewa siku ya Jumatatu na kusainiwa na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Gerson Msigwa, inasema kuwa kiongozi huyo pia ameivunja bodi hiyo kuanzia leo.

Magufuli alichukua uamuzi huo kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere na msururu wa ajali za barabarani ambazo zimesababisha vifo, ulemavu na kuharibu mali.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Siku ya Jumapili magufuli alifutilia mbali bodi ya ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme TAMESA na kumfuta kazi mwenyekiti wake John Ndunguguro kwa sababu kama hizo.

Tume kuchunguza chanzo cha ajali

Shughuli za uopoaji marehemu zikiendelea eneo la tukio
Wanawake wakisubiri miili ya wapendwa ufuoni

Waziri mkuu Kassim Majaliwa tayari ametangaza tume ya watu saba ambayo itaanza uchunguzi kuhusiana na kile kilichosababisha kuzama kwa MV Nyerere ambayo kufikia sasa imesababisha vifo vya abiria 227 ambao walikuwa wakiabiri feri hiyo.

Tume hiyo inaongozwa na afisa mstaafu wa jeshi na mbunge wa upinzani kutoka eneo hilo Joseph Lukundi miongoni mwa wengine.

Tume hiyo imepewa mwezi mmoja kukusanya ripoti na kuiwasilisha kwa rais.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Wakati huohuo, waziri huyo amefichua kwamba serikali imeanza mipango ya kutengeza feri mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba watu 200 na tani 50.

Kufikia sasa, serikali tayari imewakamata maafisa kadhaa waliokuwa wakifanya kazi katika feri .

Meli itakayoivuta MV Nyerere yawasili

Baadhi ya waogeleaji waliokuwa wakisaka miili ya watu waliofariki na walionusurika

Tayari meli iliokuwa ikibeba vifaa vitakavyotumika kuitoa kenye maji MV Nyerere imewasili katika eneo la Bwisya katika kisiwa cha Ukara, Wilayani Ukerewe.

Kamishna wa Mwanza John Mongella alisema siku ya Jumapili kwamba meli hiyo itatolewa na wataalam kutoka kwa kikosi cha uokozi wa majini.

Amesema kuwa uokozi wa chombo hicho pia utasaidia kunusuru mali iliokwama chini ya mabaki ya chombo hicho.

Hotuba ya Magufuli

MV Nyerere wakati ilipokuwa ikifanya kazi

Akizungumza moja kwa moja kupitia runinga, rais Magufuli amesema kuwa nahodha huyo tayari amekamatwa na polisi .

Aidha rais Magufuli ameagiza wale wote wanaohusika na operesheni za kivuko hicho kukamatwa ili kuhojiwa. Akihutubia taifa siku ya Ijumaa jioni rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa ana habari kwamba nahodha huyo alimwachia zamu ya kuendesha chombo hicho mtu ambaye hakuwa amepata mafunzo ya kazi hiyo.

Kulingana na Magufuli huenda sababu ya kuzama kwa chombo hicho ni 'kujaa kupitia kiasi'.

Lakini amesema kuwa kamati itakayoundwa itasaidia kutoa maelezo zaidi.

Takriban miili 160 imeopolewa kufikia sasa , kulingana na idadi ya mwisho iliotolewa kabla ya rais Magufuli kutoa hotuba yake.

Mustakabali wa mashirika yaliowekeza katika uzazi wa mpango Tanzania?

Magufuli alisema: Ni wazi kwamba miili zaidi imekwama ndani ya chombo hicho, Ripoti nilizopoikea zinaonyesha kuwa hata mizigo iliobebwa ilikuwa zaidi ya kiwango cha tani 25 zinazoruhusiwa.

Kulikuwa na tani za mahindi, kreti za pombe, vifaa vya umeme na Ujenzi. Abiria pia walikuwa wamebeba mizigo mikubwa kwa kuwa walikuwa wanatoka katika soko.