DCJ: Philomena Mwilu: Kesi ya Naibu Jaji Mkuu yasimamishwa Kenya

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu (Katikati)

Chanzo cha picha, YASUYOSHI CHIBA

Maelezo ya picha, Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu (Katikati)
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mahakama Kuu Kenya imesimamisha uendeshaji wa kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu.

Mwilu amewasilisha ombi katika mahakam hiyo akiomba asijibu mashtaka ya ulaghai, utumiaji mbaya wa mamlaka na kukwepa kulipa kodi, kesi iliyowasilishwa dhidi yake hapo jana na mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kupitia wakili wake, Okongo Omogeni, Mwilu ameambia Mahakama Kuu leo asubuhi kwamba kesi hiyo iliyowasilishwa dhidi yake ina hila na ni njama dhidi yake.

Katika ombi lake mahakamani, alikuwa amewashtaki mkurugenzi wa mashtaka ya umma, Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Mwanasheria Mkuu na Hakimu Mkuu anayeangazia kesi za ufisadi.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji
Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji

Mahakama ya juu sasa imeamua kusitisha kesi ya uhalifu inayomkabili Mwili kukisubiriwa kuamuliwa masuala ya kikatiba yanayotokana na ombi alilowasilisha Okotoba 9.

Jaji Chacha Mwita wa mahakama kuu ameeleza kwamba ombi hilo la Mwilu linazusha masuali makuu.

Naibu jaji mkuu huyo anakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo kutumia vibaya mamlaka yake, na kutolipa ushuru.

Inadaiwa kuwa jaji huyo alikiuka sheria ya uongozi na maadili kwa kupokea mkopo wa kibinafsi wa thamani ya takriban $120,000 kutoka kwa benki ya Imperial.

Mwilu hatahivyo amejitetea kwa kusema mkopo huo ulitokana na makubaliano ya kibiashara.

Mahakama hiyo kuu imeamua sasa kwamba kuna masuala ya kutathminiwa kikatiba kubaini iwapo makubaliano ya kibiashara baina ya mtu na taaisis ya kibiashara yanaweza kutazamwa kama mashtaka ya uhalifu.

Kwa sasa kesi hiyo ya uhalifu imesimamishwa hadi Oktoba 9.

Hatua hii ina maana gani kisheria?

"Mawakili wa jaji Mwili waliuliza je kuna kosa la jinai katika kukosa kulipa ushuru? ushuru si kazi ya polisi bali kazi ya Kenya Revenue Authority, yaani kile kitengo cha Kenya cha kukusanya ushuru. Kwa hivyo hilo ndilo tetesi la kwanza. Tetesi la pili ambalo walichukua pale mahakamani ni kwamba naibu jaji mkuu alichukua mkopo kutoka benki na hakuweza kupeana dhamana, wakauliza makubaliano ya benki na kupeana taratibu za kutoa mkopo ni vitu ambavyo havimo mikononi mwa polisi. Kwa hivyo hayo maswali mawili ndiyo yaliulizwa pale kotini na kusema kuwa yale mashtaka yanakiuka kanuni za kikatiba," kulingana na mwanasheria Danstan Omari alipozungumza na BBC.

Hata hivyo kesi ilisimamishwa kufuatia kuwepo dosara kwenye namba za faili za kesi. Kesi hiyo sasa imesimamishwa hadi tarehe tisa mwezi Oktoba. Hii ina maana kuwa jaji Mwilu yuko huru kuendelea na kazi zake kama kawaida akisubiri uamuzi wa mahakama ya juu. Baada ya dhamana yake aliyoweka mahakamani kukamilika siku ya Ijumaa atakuwa tena huru kuendelea na kazi zake kama naibu jaji mkuu.