Utafiti: Uchafuzi wa hewa unawaathiri wanaume zaidi China

Chanzo cha picha, Getty Images
Utafiti mpya kutoka nchini China unasema kwamba mlipuko wa muda mrefu unaweza kusababisha uchafuzi wa hali ya hewa.
Watafiti wanaamini kwama matokeo mabaya huongezeka kwa kutegemea umri wa mtu au kiwango cha elimu,na hii uleta madhara makubwa zaidi kwa wanaume wenye kiwango kidogo cha elimu.
Kwa zaidi ya miaka minne,watalamu wa hesabu na maandishi waliwafanyia utafiti watu elfu ishirini wa nchini China kwa kutumia viwango vya Marekani na China.
Watafiti wanaamini kwamba matokeo hayo yanawiana kimataifa,kwa asilimia zaidi ya 80 ya watu wakaao mjini wanavuta hewa ambayo sio salama.
Hata hivyo wakati wa kuhusisha uwiano kati ya uchafuzi wa hali ya hewa na matokeo madogo ambayo yamepatikana yataweza kuthibitisha chanzo na matokeo.
Utafiti huu unajumuisha hatua ambazo watafiti kutoka Ubelgiji katika chuo kikuu cha Peking pamoja na chuo kikuu cha Yale kilichopo nchini Marekani.
Haijafahamika bado ni kiwango gani ambacho kila anayechafua hali ya hewa analaumiwa kuchangia?
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO) linasema uchafuzi wa hali ya hewa unakadiriwa kusababisha vifo visivyotarajiwa milioni saba kila mwaka duniani kote.
"Tumetoa ushahidi wa namna ambavyo uchafuzi wa hali ya hewa unavyoleta madhara kulingana na umri wa watu haswa kwa jinsia ya kiume na watu wasio na elimu ya kutosha,"utafiti huo uliandikwa katika jarida la jumatatu lililoangazia elimu ya sayansi.
Uchafuzi wa hali ya hewa inaongeza hatari ya ongezeko la magonjwa ya kuambukiza.
Mmoja wa watafiti hao aliiambia BBC kwamba utafiti walioufanya umeweza kubainisha madhara ya uchafuzi wa hali ya hewa kulingana na umri,hivyo matokeo waliyoyapata katika maisha ni mapya

Katika tafiti yao,kati ya watu ambao walikuwa na jinsia moja waliokuwa na ummri wa kumi na kuendelea mwaka 2010 na mwaka 2014
Utafiti uliopita ulibaini kuwa uchafuzi wa hali ya hewa ulisababisha wanafunzi kpunguza uwezo wao wa kufikiri au kuelewa mambo.
Kazi za maeneo ya wazi
Wachafuzi wengi wa hali ya hewa wanafikiriwa kuwa wanaathiri ubongo kwa namna mbalimbali.
Wachafuzi wa hali ya hewa wanaweza kusababisha madhara ya kisaikolojia na kuongeza hatari ya msongo wa mawazo.
________________________________________
Uchafuzi wa hali ya hewa duniani
Watu wapatao milioni saba wanakufa kila mwaka kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa
Mwaka 2016,Uchafuzi wa hali ya hewa ulisababisha vifo milioni 4.2 duniani kote
Asilimia 91 ya idadi ya watu duniani wanaishi katika mazingira ambayo muongozo wa shirika la afya duniani katika ubora wa hewa umezidi kiwango chao.
Miji 14 nchini India ikiongozwa na Kanpur ni miongoni mwa miji 20 ambayo ina uchafuzi wa hali ya hewa duniani.
Watu tisa kati ya 10 duniani kote wanavuta hewa isiyo safi.
Source: World Health Organization
________________________________________

Chanzo cha picha, AFP
Sababu moja ambayo watafiti wameeleza kwamba wanaume wenye umri mkubwa ambao wana kiwango kidogo cha elimu wanaathirika zaidi na mlipuko wa uchafuzi wa hali ya hewa kwa sababu wao huwa wanafanya kazi za nje zaidi
Tafiti zao pia zimebaini madhara ambayo yanasababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa unaathiri utambuzi wao wa mambo kwa kiwango kikubwa zaidi ilivyokuwa inafikiriwa.
Kwa watu wenye umri kati ya 55 mpaka zaidi ya 65 madhara yake yanaweza kuwa vigumu sana kupunguza kutokana na kuepo kwa muda mrefu
Hali hii inatia hofu sana kwa sababu kila mtu amnafahamu kwamba ni lazima kila mtu afanye kazi ili aweze kupata kipato chake ,labda ni wakati wa kuangalia ni lini tunapaswa kupumzika kufanya kazi na kupanga mipango ya bima ambayo ni mizuri.
Licha ya kuwa matokeo hayo ya utafiti ni ya China lakini kiuhalisia majibu hayo yanawiana na maeneo mengine ya nchi zinazoendelea ambazo wanakabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa.
Waandishi wameonesha kuwa asilimia 98 ya miji ambayo ina watu zaidi ya laki moja ambao wana kiwango cha kati cha kipato chao na wanashindwa kufikia muongozo wa hewa safi ambao shirika la afya duniani umeweka.












