Ufugaji wa nyuki watunza msitu Zanzibar

Mfugaji wa nyuki akitembea msituni

Jurre Rompa ni mpiga picha ambaye ametumia miezi mitatu ya mwanzoni mwa mwaka 2018 kupiga picha zinazoonyesha msitu uliopo Zanzibar.

Katika safari yake kisiwani Unguja na Pemba ,bwana Rompa alipiga picha ya kikundi cha wanakijiji ambao ni wafugaji wa nyuki wakiwa wanahifadhi mizinga yao katika msitu huo.

Visiwa hivi viwili vina maeneo ya kufugia nyuki ambayo yako maili 30 kutoka katika ufukwe wa bahari ya hindi.

Msitu huo uliokuepo katika kisiwa cha Zanzibar haujaweza kuwa katika hali nzuri kutokana na kilimo cha viungo ambacho ni maarufu katika kisiwa hicho.

Kutokana na kilimo hicho maarufu kisiwani humo ,rotuba ya ardhi ya udongo wake imeonekana kutokuwa nzuri.

Kuna miradi kadhaa ambayo inaendelea ili kuurejesha msitu huo katika hali yake ya awali.

moshi unaotoa nyuki

Ufugaji wa nyuki ikiwa ni moja ya njia itakayoweza kurutubisha mimea na kufanya jitihada za kurejesha msitu kurudi kwenye hali yake ya awali.

Pamoja na kwamba wanakijiji wanatoa mchango mkubwa kufanikisha jitihada hizo,ufugaji wa nyuki unawasaidia wanakijiji kuongeza kipato chao kwa kuuza asali.

Hivyo wakulima hawa wadogo wameweza kutengeneza namna mpya ya kujipatia kipato licha ya kuathirika kwa kushuka kwa soko la karafuu na viungo ambavyo vinalimwa katika kisiwa hicho.

Salum Ali Makame akiondoa mzinga kwenye mti

Ali Manguja mwenye umri wa miaka 60 ni mkulima wa mbogamboga ambaye amekuwa akihifadhi nyuki tangu akiwa mdogo na amekuwa akitumia kipato anachokipata kwa kuuza asali kwa kulipia bili ya maji ambayo nnatumia kumwagilia mbogamboga zake.

wafugaji nyuki wakivuna asali
Maelezo ya picha, Wafugaji nyuki wakivuna asali

Kipato cha ziada ambacho anakipata anakitumia pia kuwahudumia watoto wake 11 .

Na mzee huyo alimwambia bwana Rompa kwamba atafanya shuguli hiyo mpaka Mungu atakapomtaka aache na akiwa hana uwezo kwa kuzifanya shughuli hizo tena.

wafugaji wa nyuki
Asali ikitolewa

Wakati Mohamed Abdula Mshiti mwenye umri wa miaka 57 ni mwanaume mfugaji mwingine wa nyuki ambaye anategemea kupata kipato chake cha ziad kutokana na ufugaji huo.Bwana Mohamed amekuwa mkulima kwa zaidi ya miaka 30.

Mohamed Abdula Mshiti in his beekeeping outfit
Maelezo ya picha, Mohamed Abdula Mshiti ni mfugaji wa nyuki
Raymond Kilango and Juma Salim Mussa

Lita moja ya asali inauzwa kwa shilingi za Tanzania 24,000/ au dola 10.5.

Asali inatumika kwa ajili ya kula na inatumika kama dawa.

"Kama unaweza kula kijiko kimoja cha asali asubuhi na unaweza usijisikie njaa siku nzima."

Picha hizi zimepigwa na Jurre Rompa