Mamilioni ya watu wanakaa kwenye kambi na wengine maelfu wamekwama kwenye mafuriko nchini India

Takribani watu 400 wamekufa na wengine maelfu wamekwama katika mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kutokea kabla katika karne hii huko India katika mji wa Kerala.

Watu zaidi ya milioni moja hawajulikani walipo na wengine maelfu wanaishi kwenye kambi.

Mvua kubwa za masika zinazosababishwa na upepo mkali zilipoanza,jitihada nyingi zilifanyika ili kuwaondoa watu katika maeneo hayo ya pembezoni.