Uchaguzi Marekani: Microsoft yadai imewashinda wadukuzi wa mtandao kutoka Urusi

Jitihada za Urusi kutaka kufanya shambulizi la uhalifu katika mitandao dhidi ya Marekani zimetibuka, Microsoft imesema.

Kampuni hiyo ya Komputa imesema wadukuzi hao kutoka Urusi walikuwa wanajaribu kuiba kutoka kwenye makampuni ya kisiasa ambayo yanajumuisha taasisi za kimataifa za Republican pamoja na Hudson think tanks.

Lakini mipango hiyo ilishindwa kufanikiwa baada ya wafanyakazi wa usalama kufanikiwa kuthibiti tovuti zao.

Microsoft inasema kundi la 'Fancy Bear'udukuzi linausika katika hilo shambulizi.

Miliki ya tovuti

"Tuna hofu juu ya majaribio kama haya na mengine yanayotoa vitisho vya usalama katika makundi ambayo yanahusiana na vyama vya kisiasa vya Marekani katika kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2018" Microsoft ilisema hayo katika blogu inayoeleza kazi inazozifanya.

Microsoft iliongeza kwa kusema kwamba mashambulizi hayo yaliyoshindikana yalikuwa na uwezekano wa kuanza kwa kampeni ambayo ingehusisha kuwapotosha watu kutembelea katika miliki za tovuti ambazo kundi hilo lingeweza kuona na kuiba taarifa za watu.

Hata hivyo Urusi ilikana shutuma ambazo Microsoft imezitoa ambazo zimewalenga na kudai kuwa kampuni ya Microsoft inafanya kazi kama wapelelezi badala ya kuw kampuni binafsi.

Microsoft inafanya mchezo wa kisiasa,taarifa hizo zilisemwa na mtu ambaye hakujitambulisha.Uchaguzi bado haujafanyika lakinitayari kumekuwa na shutuma.

Gazeti la New York Times linadhani kwamba kundi la think tanks lilikuwa limelengwa kwa sababu wallikuwa wafuasi wa rais Donald Trump lakini bado wapinzani nguvu kubwa inabidi iwekwe kwa Urusi.

Aidha mpaka sasa hakuna ushaidi wowote ambao unaonesha kwamba kulikwa na ushambulizi wa miliki za tovuti.

Microsoft ilieleza pia kwamba shambulio la namna hiyo katika tovuti linatoa picha ya kile kilichoonekana mwaka 2016 nchini Marekani na kwenye uchaguzi wa Ufaransa mwaka 2017.

Hatua hiyo iliyofanywa na Microsoft imekuja mara baada ya Marekani kubadili maafisa wake12 wa kijasusi kudukua mtandao uliotumiwa na Hillary Clinton na chama cha Democratic.

Urusi imesisitiza kukana juu ya kufanya ushambulizi wa udukuzi uchaguzi wowote na katika taasisi za nchini Marekani.