Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner yawasili Tanzania

Ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imewasili nchini Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa sasa anawangoza raia wa taifa hilo katika sherehe ya mapokezi ya ndege hiyo.
Ndege hiyo imetua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ikitokea mjini Seattle Marekani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliochapishwa awali na Mkurugenzi wa mawasiliano katika Ikulu ya rais, ndege hiyo ni ya nne kuwasili nchini humo kati ya saba zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania {ATCL} kuimarisha huduma zake.
Ndege hiyo ina uwezo kubeba abiria 262.
Ndege nyingine ambazo zilinunuliwa na serikali ya Tanzania ni ndege moja aina ya Bombardier Q400 Dash 8 NextGen , ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 .

Mwaka 2016 Tanzania ilipokea ndege mpya ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) katika hatua ya kuimarisha safari za ndani ya nchi za shirika hilo.
Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) kutoka Canada ilikotengenezewa.
Rais Magufuli alikuwa ameahidi kwamba shirika hilo lingeimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani.

Baadhi ya maeneo ambayo ATCL inatarajia kuongeza safari zake ni Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma, Tabora, Mpanda, Kilimanjaro, Mtwara, Zanzibar, Pemba, Bukoba na Visiwa vya Comoro.
Kulingana na Boeing, 787 Dreamliner ni familia yenye teknolojia ya kisasa ,ndege zenye utendaji mzuri na vitu vipya vya kupendeza.

Mbali na kuleta vigezo vya ndege kubwa katika ndege za wastani, 787 Dreamliner italipatia shirika la ndege la Air Tanzania ufanisi wa mafuta na mazingira ya utendaji, kwa kutumia chini ya asilimia 20 hadi 25 ya mafuta na asilimia 20 hadi 25 wa uchafuzi wa mazingira ikilinganishwa ndege nyengine zilizotumika awali.













