ACT Wazalendo: Serikali ya Tanzania inataka kuminya haki zote za msingi za raia

Katibu Mwenezi wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akizungumza na wanahabari
Maelezo ya picha, Katibu Mwenezi wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akizungumza na wanahabari
Muda wa kusoma: Dakika 2

Chama cha upinzani Tanzania ACT Wazalendo kimesema mwenendo wa serikali kudhibiti mitandao ya kijamii unaonesha nia ya kutaka kuminya haki zote za msingi za raia

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi wa chama hicho Ado Shaibu amesema ''taratibu kila mtu, haijalishi ni wa chama au cheo gani, atafikiwa na ukandamizaji huu wa serikali''.

Chama cha Upinzanzi nchini Tanzania, ACT Wazalendo, kimesema kuanza kwa kutekelezwa kwa kanuni za maudhui mtandaoni ni ishara nyingine ya jinsi ambavyo serikali nchini humo inavyoendelea kuminya uhuru wa habari na watu kujieleza.

Jana mtandao maarufu wa Jamii Forums ulilazimika kufunga huduma zake baada ya kushindwa kukidhi matakwa ya kanuni hizo.

Amewataka wananchi kupaza sauti kwa pamoja kuikemea serikali kwa ukandamizaji unaoendelea.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

Katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema, kufungwa kwa mtandao huo na mingine baada ya tarehe ya mwisho wa kujisajili kufika, ni kitendo kinachoonyesha kuwa serikali haitaki kuskiliza maoni ya wananchi kuwa kanuni hizo ni kandamizi kwa uhuru wa habari na watu kujieleza.

''Kauli yetu ni kwamba serikali ya awamu ya tano tusitarajie asilani, abadan kwamba itakoma kukandamiza haki za binaadamu.Inaonekana waziwazi serikali taratibu inaua haki moja mpaka haki nyingine kwa hiyo katika kitu tunachopoteza muda ni kudhani kuwa tukitoa rai kwa serikali basi ati watatusikiliza, imethibitika kuwa hawatusikilizai na haki nyingi zimesombwa na maji'',Alieleza Ado.

Jamii Forums, mtandao ambao uliokuwa na watumiaji zaidi ya Laki 6 kila siku na wafuasi zaidi ya Milioni tatu katika mitandao yake ya Kijamii ulikuwa ni jukwaa ambalo Watanzania walilitumia kubadilishana mawazo, kutoa habari na mara nyingine kuikosoa serikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa nyeti.

Wakati serikali ikiutaka mtandao huo kujisajili, Jamii Forums wenyewe wamekuwa wakisisitiza kwamba sharti hilo haliwahusu kwani wao si watoa maudhui bali ni wananchi wanaoutumia mtandao huo kwani wao ndio wanaweka humo maudhui ya mtandao huo

Wanaharakati wengi wa maswala ya haki za binaadamu wamekosoa sheria na kanuni za mtandao kuwa ni kandamizi kwa uhuru wa habari na kujieleza nchini.