Marekani: Mazungumzo na Korea Kaskazini yamepiga hatua kubwa

Chombo cha habari cha Korea Kaskazini
Maelezo ya picha, Chombo cha habari cha Korea Kaskazini
Muda wa kusoma: Dakika 2

Marekani inasema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini yanaendelea kwa kasi kabla ya kufanyika kwa mkutano kati ya viongozi wa mataifa hayo mawili siku ya Jumanne.

Mazungumzo hayo kati ya maafisa yamekuwa yakifanyika kabla ya mkutano wa kwanza.

Ikulu ya Whitehouse pia imethibitisha kwamba rais Trump na Kim Jong un watafanya mazungumzo ya ana kwa ana huku wakalimani pekee wakiruhusiwa.

Matokeo ya mkutano huo yatabaini hatma ya mpango wa kinyuklia wa Iran.

Marekani inasisitiza kuwa haitakubali chochote isipokuwa kusitisha mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini imesema kuwa iko tayari kusitisha mpango wake wa kinyuklia lakini ikaongezea kuwa swala hilo litategemea na tafsiri ya neno hilo.

Bado haijulikani ni nini Korea kaskaini itahitaji kufanyika , swala linalofanya mkutano huo kuwa bvigumu kubashiri kulingana na wachanganuzi.

Rais kim Jong un akisalimiana na raia katika hoteli moja nchini Singapore
Maelezo ya picha, Rais kim Jong un akisalimiana na raia katika hoteli moja nchini Singapore

Usiku kabla ya siku hiyo kuu

Huku usiku ukitanda , bwana Kim amefanya ziara isio ya kawaida katika maeneo ya mji huo.

Aliwapungia mkono watazamaji ambao walimfurahikia alipokuwa akiwasili katika hoteli moja mjini humo.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Singapore Vivian Balakrishnan pia alituma ujumbe wa Twitter uliokuwa na neno "jalan-jalan", neno linalotumika nchini humo kumaanisha tembea tembe katika bustani zilizpo

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Yeye na rais Trump wanaishi katika hoteli tofauti , ambazo hazina umbali mrefu kati yao.

Usalama umeimarishwa katika eneo hilo. Viongozi hao wawili watakutana siku ya Jumanne katika hoteli ya Sentosa, kisiwa maarufu cha wataalii kilichopo mita chache karibu na taifa la Singapore.

Viongozi wote wawili wana 'matumaini'

Bwana Balakrishnan, ambaye alikutana na Trump na Kim mbalimbali siku ya Jumapili jioni aliambia BBC kwamba viongozi wote wawili walikuwa na matumaini chungu nzima.

rais Trump amasema kuwa anahisi vyema kuhusu mkutano huo wa siku ya Jumanne.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Bwana Balakrishnan alithibitisha kuwa Singapore itaulipia ujumbe wa Korea Kaskazini ikitaja hatua hiyo kuwa ukarimu ambao imejitolea kufanya

Map showing location of summit on Sentosa in Singapore

Ajenda ya mkutano ni ipi?

Kulingana na Ikulu ya Whitehouse huu ndio mpango wa mkutano huo.

  • Bwana Trump na Bwana Kim watasaliamia (9am local time)
  • Mkutano wa ana kwa ana
  • Mkutano wa pamoja na wawakilishi wengine.
  • Chakula cha mchana

Bwana Trump ataondoka nchini humo jioni hiyo hiyo kurudi nchini Marekani.

Rais Kim Jong un na mwenzake wa marekani Donald Trump wanatarajiwa kufanya mazungumzo hapo kesho
Maelezo ya picha, Rais Kim Jong un na mwenzake wa marekani Donald Trump wanatarajiwa kufanya mazungumzo hapo kesho

Je Korea Kaskazini imesemaje?

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini tayari vimeanza kuripoti kuhusu ziara ya rais Kim nchini Singapore kukutana na rais Trump .

Kisheria wanapaswa kuripoti kuhusu ziara za kiongozi huyo baada ya mkutano huo.

uhariri wa gazeti moja nchini humo pia umezungumzia kuhusu 'uhusiano mpya na Marekani'.

Marekani imesema nini?

Mike Pompeo, mjumbe mkuu wa rais Donald Trump , amesema kuwa rais amejiandaa vilivyo kwa mkutano huo .

Amesema kuwa marekani itaridhika na kusitishwa kwa mipango ya kinyuklia katika rasi ya Korea- huku ukaguzi ukiwa ndio muhimu katika makubaliano yoyote