Mama wa Jay-Z: Nilimwambia mwanangu nina mpenzi wa jinsia moja

Jay-Z alifahamu kuwa mama yake anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jay-Z alifahamu kuwa mama yake anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Mama yake mwanamuziki maarufu nchini Marekani na duniani, Jay- Z amezungumza namna ambavyo mtoto wake amekuwa akimpa moyo alipomwambia kuwa amekuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Gloria Carter aliiambia hadhira katika tuzo za GLAAD kuwa ni mara ya kwanza kuzungumza na mtu kuhusu ukweli wake

Mama wa watoto wanne alitunukiwa tuzo akitambuliwa kwa mchango wake kwenye wimbo uitwao Smile uliotolewa mwaka jana.

Alisema: ''Smile imekuwa halisia kwa sababu nilimshirikisha mtoto wangu nikimweleza mimi ni nani.''

''Mtoto wangu alilia na akasema: 'lazima maisha yalikuwa mabaya sana kuishi namna hiyo kwa muda mrefu.''

''Maisha yangu hayakuwa mabaya,''aliongeza.

''Nilichagua kuilinda familia yangu.Nilikuwa na furaha japo sikuwa huru.

Tuzo za GLAAD Media zinawatambua watu na taasisi kwa kazi zao katika kuwakilisha jamii ya watu wanaojihusisha na mapanzi ya jinsia moja na maswala yanayoathiri maisha yao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tuzo za GLAAD Media zinawatambua watu na taasisi kwa kazi zao katika kuwakilisha jamii ya watu wanaojihusisha na mapanzi ya jinsia moja na maswala yanayoathiri maisha yao

Awali Jay-Z alieleza namna alivyolia kwa furaha baada ya mama yake kuzungumza naye kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Katika wimbo wake katika albamu yake mpya ya 4.44 anasema ''Mama alikuwa na watoto wanne, lakini ni alikuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, alijificha kwenye kabati, maumivu yake hayakuweza kuvumilika

Alikiambia kipindi cha US talk show kinachoongozwa na David Letterman ''kwa mama yangu kuishi akijifanya kuwa mtu ambaye siye, akijificha , kulinda watoto wake-akiogopa kuwaaibisha miaka yote hii, kwa yeye kuniambia ''Nafikiri nampenda mtu fulani''. Nililia sana,'' Jay Z alikiambia kipindi hicho.

Alisema siku nyingi alifahamu mama yake anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, lakini wawili hao walizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu swala hilo mwaka jana.

Mazungumzo yao yalikuja wakati Jay-Z alipokuwa akitengeneza albamu yake mpya ya 4.44

''Ilikua ni mara ya kwanza tulizungumza na kwa mara ya kwanza nilimsikia akisema anampenda mwenza wake (wa jinsia ya kike) Alieleza Jay-Z.