Binyavanga Wainaina: Mkenya mpenzi wa jinsia moja kufunga ndoa na raia wa Nigeria

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Mwandishi vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina ambaye ametangaza wazi kwamba ni mpenzi wa jinsia moja amefichua kwamba atafunga ndoa mwaka ujao.
Mwandishi huyo ambaye alifichua hali yake ya kimapenzi mwaka 2014 siku yake ya kuzaliwa akiwa na umri wa miaka 2014 amesema harusi hiyo itafanyika nchini Afrika Kusini.
"Nilimuomba mpenzi wangu tufunge ndoa wiki mbili zilizopita. Na alikubali, karibu mara moja. Yeye ni raia wa Nigeria. Tutakuwa tunaishi Afrika Kusini ambapo atakuwa anahudhuria masomo mwaka ujao. Tutaoana huko, mapema mwaka ujao," Bw Wainaina aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Aliahidi kwamba kutakuwa na karamu kubwa kwa Wakenya jijini Nairobi mwaka ujao.
Baadaye, aliongeza kwamba ana uhakika kutakuwa na sherehe kubwa kwa Wanigeria pia.
"Hakuna lililonishangaza zaidi kuliko kupendana na mtu huyu, ambaye ni mpole na mwenye moyo wa ukarimu.
"Najichukulia kuwa mwenye bahati sana kwamba yeye ananipenda na tulipendana majuzi tu, lakini tumefahamiaka na tumekuwa tunachumbiana tangu 2012."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Bw Wainaina alifichua kuwa yeye ni mpenzi wa jinsia moja mwaka 2014 kwenye makala aliyoipa jina „Mimi ni mpenzi wa jinsia moja, mama."

Binyavanga ni nani?
- Kenneth Binyavanga Wainaina ambaye ana umri wa miaka 47 sasa ni mwandishi wa vitabu na mwanahabari.
- Mwaka 2002 alishinda tuzo mashuhuri ya uandishi kuhusu Afrika ya Caine.
- Jarida la Time mwaka 2014 lilimuorodhesha Wainaina kuwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.
- Mnamo 1 Desemba, 2016 alitangaza kupitia Twitter Siku ya Ukimwi duniani kwamba alikuwa ana virusi vya Ukimwi.













