Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kipchoge aibuka kidedea London Marathon
Mkenya Eliud Kipchoge, aibuka ameibuka kidedea katika mbio za Marathoni za London wa mara ya tatu.
Kipchoge ni moja kati ya wakimbiaji hodari ambae alianza vyema mbio hizo akitumia muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 27.
Mwingereza Mo Farah alikuwa akiongoza katika hatua za awali kabla ya kupoteza mwelekeo na kumaliza katika nafasi ya tatu dakika tano nyuma ya Kipchoge.
Mkiambiaji toka nchini Ethiopia Tola Shura Kitata amemaliza katika nafasi ya pili akiwa nyuma kwa sekunde 33 dhidi ya Kipchoge.
Vivian Cheruiyot wa Kenya alishinda kwa upande wa wanawake kwa kutumia muda vizuri katika mashindano.
Wakimbiaji zaidi ya 40,000 walishiriki katika mashindano hayo ya London Marathon katika kipindi cha joto zaidi katika mwaka.