Mwanamume ajipiga risasi na kujiua nje ya White House

Police outside the White House front lawn - 3 March 2018
Maelezo ya picha, Polisi nje ya White House

Mwanamume mmoja amejipiga risasi na kujiua nje ya Ikulu ya Marekani ya White House mjini Washington, kikosi cha kumlinda rais kimesema

Kikosi hicho kilisema kuwa mwanamume huyo alikaribia ua unaozunguka Ikulu katika barabara ya Pennsylvania kabla ya kuchomoa bunduki na kupiga risasi mara kadhaa.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa, kulingana na polisi.

Rais Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu. Yuko katika kasri lake la Mar-a-Lago huko Florida.

People running at the White House

Chanzo cha picha, Twitter/@FlorianLuhn/via Reuters

Maelezo ya picha, Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo

Mwanamume huyo alikuwa kwenye watu wengi wakati alipiga risasi, kulingana na wale walioshuhudia.

Video iliyochapishwa kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha watu wengi wakikimbia kutoka eneo hilo.

Jina na mtu huyo bado halijatangazwa.

Kumekuwa na visa kadha vinavyohusu usalama katika Ikulu ya White House miaka ya hivi karibuni.

Cha hivi karibuni tarehe 23 Februari, gari liliendeshwa kwenda kwa kizuizi cha Ikulu ambapo mwanamke wa miaka 35 alikamatwa.

Tourists mill outside the north fence of the White House

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kisa hicho kilitokea karibu ua wa Ikulu