Watu 12 wafariki kwenye ajali ya barabarani Tanzania

Watu 12 wafariki kwenye ajali ya barabarani Tanzania

Chanzo cha picha, Athumani Makoye

Maelezo ya picha, Watu 12 wafariki kwenye ajali ya barabarani Tanzania

Watu 11 wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiece kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya biharamulo mkoani kagera.

Gari hilo lilikuwa linasafiri kutoka wilaya ya kibondo kuelekea kahama mkoani Shinyanga

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera Bw Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya biharamulo kwenda kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa hiece na utingo wake ni miongoni mwa waliofariki.

Bw Kayuki amesema hiece hiyo ilikuwa ikitokea kibondo kwenda kahama ambapo malori yaliyohusika kwenye ajali hiyo yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika