Kwa Picha: Uchaguzi wa marudio Kenya 26 Oktoba
Uchaguzi wa urais wa marudio ulifanyika nchini Kenya leo ambapo idadi ya waliojitokeza kushiriki ilikuwa chini ukilinganisha na uchaguzi wa tarehe 8 Agosti.

Mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia na alikuwa amewahimiza wafuasi wake kususia.
Ingawa upigaji kura uliendelea vyema ngome za serikali, katika ngome za upinzani uchaguzi ulitatizika kutokana na maandamano na makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa Bw Odinga.
Uchaguzi katika majimbo manne umeahirishwa hadi Jumamosi na tume ya uchaguzi.
Huu hapa ni mseto wa picha za hali ilivyokuwa maeneo mbalimbali nchini humo.
Tuanze na mwanamume huyu katika eneo la Katwekera katika mtaa wa Kibera, Nairobi ambaye alijipata amezingirwa na maafisa wa polisi.

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya waandamanaji. Mwanamume huyu alirushiwa bomu la kutoa machozi Kibera.

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Hapa chini ni masanduku ya kupigia kura ya eneo bunge la Kisumu ya Kati ambayo hayakusafirishwa vituoni. Eneo hilo lina vituo 196.

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Mjini Kajiado, hali ilikuwa tulivu. Mwanamke huyu anaonekana akipakwa wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura yake.

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Familia hii ilifika katika kituo cha kupigia kura cha Mutomo, Gatundu katika jimbo la Kiambu na mavazi ya kipekee - mavazi ya rangi za bendera ya Kenya.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitimiza miaka 56 hivi leo. Alizaliwa siku sawa na ya leo mwaka 1961.Watoto hawa wamekuwa kwenye kituo cha kupigia kura cha Mutomo, ambacho ndicho Bw Kenyatta, wakiwa na fulana zenye ujumbe wa kumtakia heri siku ya kuzaliwa kwake.

Rais Uhuru Kenyatta baada ya kupiga kura katika kituo cha Mutomo, Gatundu katika jimbo la Kiambu alisema wakati umefika kwa taifa hilo kusonga mbele. Hapa anaonekana akipiga picha ya selfie na mmoja wa waliokuwa kituoni.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika kituo hicho cha Mutomo, kulikuwa na mbwa huyu langoni. Alitaka kupiga kura pia?

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea na matokeo yanatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha siku saba.
Hapa ni shughuli ya kuhesabu kura katika kituo kimoja Kisumu.

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Picha kwa hisani ya AFP, Getty Images, BBC












