Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marais 5 wa zamani wakutana kuchangisha fedha Marekani
Marais watano wa zamani nchini Marekani wamekusanyika kwenye warsha ya kuwasaidia waathiriwa wa janga la kimbunga ambacho kilikumba maeneo kadha ya Marekani.
Barack Obama, George W Bush, Bill Clinton, George HW Bush na Jimmy Carter wote walikutana Texas siku ya Jumamosi.
Wedemocrat watatu wa Warepulican wawili walikutana warsha ya Amerika moja yeye lengo la kuwasaidia wale walikumbwa na janga la vimbunga Irma na Maria.
Warsha hiyo imechangisha dola milion 31 hadi sasa.
Wanasiasa hao walizindua mchango huoa baada ya kibunga Harvey ambacho kilisababisha uharibifu wa mabilioni ya fedha kilitua katika jimbo la Texas Agosti.
Mchango huo sasa utasaidia jamii za Florida, Puerto Rico na viswa vya Marekani vya Virgin vilivyopigwa na kibunga.
Hata hivyo Rais Trump hakuhudhuria, lakini alituma ujumbe kabla na kuwapongeza marais hao kwa kazi yao nzuri.
Obama na Bush awali wametoa hotuba na kuukashifu utawala wa Trump.