Mshambuliaji Stephen Paddock aua watu 58 Las Vegas, Marekani

People fleeing from scene of country music festival

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zaidi ya watu 50 wauawa kwa wapigwa risasi Las Vegas Marekani

Zaidi ya watu 58 wameuawa na takriban 515 kujeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi wakati wa tamasha la muziki huko Las Vegas, Marekani.

Mtu mwenye bunduki mwenye umri wa maika 64 Stephen Paddock alifyatua risasi kutoka ghoroga ya 32 kwenye hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa tamasha lililokuwa likiendelea nje.

Eneo la mauaji
Maelezo ya picha, Eneo la mauaji

Polisi wanasema mshukiwa ambaye alitajwa kuwa makaazi wa mji huo na ambaye hakutajwa jina ameuawa.

Mamia ya watu walikimbia eneo hilo na milio ya risasi ikasikika kwa muda kwenye video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.

Ufyatuaji huo ulitokea mwendo wa saa 05:30 GMT na walioshuhudia walisema kuwa mamia ya risasi zilifyatuliwa.

Usafiri wa ndege ulisitishwa kutoka uwanja wa ndege wa McCarran mjini Las Vegas

People fleeing from scene of shooting

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zaidi ya watu 50 wauawa kwa wapigwa risasi Las Vegas Marekani
Police are seen crouching in front of vehicle outside hotel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Polisi wakiwa nje ya hoteli ya Mandalay