Urusi: Vikosi vyetu vimeshambuliwa na vinavyoungwa mkono na Marekani ,Syria

Marekani haijazungumzia tukio hilo
Maelezo ya picha, Marekani haijazungumzia tukio hilo

Urusi imesema vikosi vyake vilivyopo nchini Syria vimeshambuliwa na waasi wanaoungwa mkono na Marekani Mashariki mwa nchi hiyo.

Inasema vikosi hivyo vilivamiwa wakati vikipambana na IS baada ya kuvuka mto Euphrates.

Kwa mujibu wa Urusi, mashambulizi haya yalitoka kwa vikosi vya Kikurdi na vya kiarabu vinavyoungwa mkono na Marekani.

Vikosi vya Syria na wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani, wanapambana kurejesha mji wa Deir ez-Zour ambao umeshikiliwa na IS.

Kuna wasiwasi kwamba huenda mapigano yakazuka baina ya wenyewe kwa wenyewe.