Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Moto wa nyika walazimu maelfu kuhamishwa Ufaransa
Moto wa nyika nchini Ufaransa umelazimu karibu watu 10,000 kuhamishwa usiku ya kuamkia leo kwa mujbu wa maafisa.
Wazima moto wametumwa kupambana na moto huo karibu na maeneo la Bormes-les-Mimoses.
Mapema Ufaransa iliiomba majirani wake wa EU msaada zaidi kupambana na moto huo.
Karibu ekari 4,000 za ardhi zimeteketea katika pwani ya Mediterranean.
Katika eneo la Corsica mamia ya nyumba zimehamwa.
Kwa ujumla wazima moto 400 na wanajeshi wanaotumia maji wanajaribu kuuzima moto huo tangu Jumatatu.
Takriban wazima moto 12 wamejeruhiwa na polisi 15 kuathiriwa na moshi kutoka kwa moto huo.