Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Moto waua watu 13 nchini Ufaransa
Moto uliozuka kwenye kilabu kimoja katika mji ulio kaskazini mwa Ufaransa wa Rousen wakati wa sherehe ya siku ya kuzaliwa ulisababisha vifo vya karibu watu 13 na kuwajeruhi wengine sita.
Mishumaa kwenye keki ndiyo ilianzisha moto huo katika klabu ya Cuba Libre, ambao ulianza saa sita usiku ,siku ya Jumamosi.
Dari la chumba ambacho kilishika ilikuwa imetengenezwa kwa plastiki,kulingana na shirika la habari la AFP
Waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve, amesema zaidi ya wazima moto 50 waliitwa kuuzima moto huo.
Kwa hivi sasa uchunguzi unaendelea.
Mtu mmoja kati ya waliojeruhiwa yuko katika hali mahututi
Swala la ujambazi limetupiliwa mbali.