Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamume ambaye kidole cha mguu kilihamishwa kwa mkono
Mfanyakazi mmoja wa shamba la ng'ombe ambaye kidole chake cha gumba kiling'olewa ana fahali, amefanyiwa upasuaji ambapo kidole chake ya mguu kilikatwa na kuhamishwa kwa kile cha mkono.
Zac Mitchell, 20, alijeruhiwa wakati akifanya kazi katika shamba moja lililo kijijini magharibi mwa Australia.
Alifanyiwa upasuaji mara mbili wa kurudisha kidole chake bila ya mafanikio kabla ya madaktari kuamua kuhamisha kidole chake cha mguu katika upasuaji uliodumu saa nane.
Bwana Mitchell alisema wafanyikazi wenake walijaribu kuhifadhi kidole mara baada ya ajali hiyo.
Mitchel alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali katika jimbo la Perth, lakini jitihada za kukiokoa kidole chake zikashindikana.
Licha ya kukataa Mitchel baadaye alikubali kidole chake cha mguu kuhamishwa hadi kwa mkono wake.
Daktari wa upasuaji Sean Nicklin anasema hakushangazwa na muda aliochukua Mitchel kukukubali.
"Hata kama una vidole vinne vilivyo vyema, na huna kidole cha kifinyilia mkono wako utakuwa umepoteza sehemu kubwa ya kazi yake.
Bwana Mitchel atahitaji zaidi ya miezi 12 ya ushauri lakini na mpango wa kurudi shambani.