Trump Junior alikutana na wakili wa Urusi baada ya kuahidiwa kumzungumzia Hillary Clinton

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwana wa kiume wa rais wa Marekani Donald Trump, alikubali kukutana na wakili mrusi baada ya kuahidiwa taarifa potovu kumhusu Hillary Clinton.
Donald Trump Junior anasema alikutana na Natalia Veselnitskaya lakinai hakuna taarifa ya maana kuhusu Bi Cliton ilitolewa.
Pia wakati wa mkutano huo alikuwawemo mkwe wa Rais Trump Jared Kushner na alikuwa mkuu wa kampeni wakati huo Paul J Manafort.
Maafisa wa Marekani wanachunguza madai ya Uruis kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.
FBI na Congeress wote wanachunguza ikiwa maafisa wa kampeni ya Trump walishiriana na Urusi
Mkutano na wakili Veselnitskaya ulifanyika tarehe 9 mwezi Juni mwaka 2016 katika jumba la Trump Tower mjini New York, baada ya Trump kupata uteuzi wa Republican.

Chanzo cha picha, Getty Images








