Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump aitaka Urusi kuwacha kuivuruga Ukrain
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito kwa Urusi kuacha kuivuruga Ukrain na nchi zingine, na kuacha kuungia mkono tawala dhalimu kami zile za Styria na Iran.
Akiongea akiwa mji mkuu wa Poland Warsaw, Trump aliitaka Urusi kujiunga na mataifa yenye kuwajibika.
Urusi imepinga matamshi hayo ya Trump.
Rais huyo wa Marekani amesafiri kuenda mjini Hamburg kuhudhuria mkutano wa G20 ambapo atakutana na rais wa Urusi kwa mara ya kwanza.
Mjini Warsaw alihutubia umati mkubwa uliokuwa ukimshangilia
Aliisifu Poland kama nchi iliyo tayari kulinda uhuru wa magharibi.
Bwana Trump aliitaka Urusi kuungana na nchi zinaowajibika katika vita dhidi ya adui mmoja.
Msemaji wa serikali ya Urusi Dmitry Peskov alisema kuwa Urusi haijakubali kuwa inavuruga eneo hilo.
Trump ametofautiana na baadhi ya nchi za ulaya kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na biashara,
Mashirika ya kutoa misaada yatarajiwa kufanya maandamano mjini Hamburg kuwakata viongozi kujitahidi zaidi kumaliza kutokuwepo usawa.