Mwanamuziki Bobi Wine akamatwa Uganda

Mwanamuziki Bobi Wine akamatwa Uganda

Chanzo cha picha, Bobi Wine

Maelezo ya picha, Mwanamuziki Bobi Wine akamatwa Uganda

Mwanamuziki ya nyimbo za reggae nchini Uganda Robert Kyagulanyi, ambaye ni maarufu kama Bobi Wine, amekamatwa kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Alikuwa akifanya kampeni kama mgombea huru kwa nafasi inayong'ang'aniwa vikalia nje ya mji wa Kampala, kwenye uchaguzi mdogo ambao utafanyika siku ya Alhamis.

Magazeti ya New Vision na Monitor yanasema kuwa hakukutolewa sababu ya kukamatwa kwake.

Lakini lile la Monitor linasema kuwa wafuasi wake walipambana na wale wa mpinzani wake jana Jumatatu.

Rais Museveni wa chama cha NRM na hasimu wake wa muda mrefu Dr. Kizza Besigye wa FDC, pia na wanatarajiwa kufanya mikutano eneo hilo leo, kuwaunga mkono wagombea wao.