Marekani yaishambulia na kuiangusha ndege isiyo na rubani nchini Syria

An F-15 Eagle jet (file image)

Chanzo cha picha, US Air Force

Maelezo ya picha, Ndege ya F-15 Eagle ikirusha kombora

Ndege ya jeshi la Marekani imeangusha ndege isiyo na rubani inayoendeshwa na serikali ya Syria kusini mwa nchi.

Ndege hiyo isiyo na rubani ilidaiwa kuwa na silaha na ilikuwa hatari kwa jeshi la Marekani ardhini.

Iliangushwa karibu na eneo la Tanf.

Hiki ni kisa cha karibuni kabisa katika anga ya Syria, baada ya Marekani kuangusha ndege ya kivita ya Syria siku ya Jumapili na ndege nyingine isiyo na rubani mapema mwezi huu.

A Shahed 129 drone

Chanzo cha picha, Iranian TV

Maelezo ya picha, Ndege ya Iran isiyo na rubani

Kuangushwa kwa ndege hiyo inaongeza msukosuko uliopo eneo hilo.

Katika taarifa nyingine jeshi la Marekani lilitangaza rasmi kuwa lilimuua kiongozi wa cheo cha ju wa kundi la Islamic State Turki al-Binali, wakati wa shambulizi lililofanywa na ndege nchini Syria Mwezi uliopita.

BBC map
Maelezo ya picha, Syria