Afrika pichani wiki hii : 26 Mei - 1 Juni 2017

Polisi wa kike wa Nigeria akiamrisha gwaride mbele ya maafisa na umma wa Nigeria wakati wa sherehe za siku ya Demokrasia Mei 29, 2017 katika medani ya Freedom uhuru huko Owerri. Democracy Day ni maadhimisho ya kumalizika kwa utawala wa kijeshi nchini Nigeria Mei 1999.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumatatu, polsi wa kike wa Nigeria Monday,akionesha ukakamavu wake katika siku ya sherehe za siku ya Demokrasia - ambayo ni kumbu kumbu ya kumalizika kwa utawala wa kijeshi
Olufunke Oshonaike wa Nigeria akishiriki mashindano ya kimataifa ya mchezo wa tennis kwa wanawake ya Women Single 1. katika eneo la Messe huko Duesseldorf Ujerumani 31, Mei 2017

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Olufunke Oshonaike wa Nigeria akishiriki mashindano ya wanawake ya Women Single 1 Round katika mashindano ya dunia ya mchezo wa Tennis World nchini Ujerumani Jumatano
Emmanuel Rutema, Mtanzania mwenye ulemavu wa ngozi ambaye mkono wake ulikatwa kwa imani za kishirikina , akijaribu kuvaa mkono bandia katika hospitali ya Shriners huko Philadelphia

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jumanne , Mtanzania Emmanuel Rutema akijaribu kuvaa mkono bandia baada ya mkono wake kukatwa na mtu ambaye alitaka mkono wa mlemavu wa ngozi kwa sababu zenye imani ya utata
Kituo cha safari za Leri cha Mombasa

Chanzo cha picha, Michael Khateli

Maelezo ya picha, Kituo cha udhibiti wa safari za Leri cha Mombasa Kenya kinachofanana na cha safari za anga kilizinduliwa kwa ajili leri mpya iliyojengwa na wachina Jumatano
Jumamosi , rais wa Kenya President Uhuru Kenyatta, rais wa Guinea Alpha Conde, rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Akinwumi Adesina, Makamu rais wa Nigeria Yemi Osinbajo na Waziri Mkuu wa Ethiopian Hailemariam Desalegn (Lkushoto kuelekeaa kulia) wato wakiwa wamesimama kwa ajili ya kupiga picha na rais wa Marekani Donald Trump katika kikao cha G7 Mei 27, 2017 mjini Taormina, Sicily

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumamosi , rais wa Kenya President Uhuru Kenyatta, rais wa Guinea Alpha Conde, rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Akinwumi Adesina, Makamu rais wa Nigeria Yemi Osinbajo na Waziri Mkuu wa Ethiopian Hailemariam Desalegn (Lkushoto kuelekeaa kulia) wato wakiwa wamesimama kwa ajili ya kupiga picha na rais wa Marekani Donald Trump katika kikao cha G7.
Wanaounga mkono uhuru wa -Biafra wakiandamana Mei 30, 2017 mjini Abidjan, wakati wa maadhimisho ya 50 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Nigeria

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bwana Trump pia ana mashabiki kusini mashariki mwa Nigeria, ambako baadhi ya watu waliadhimisha miaka 50 tangu kutangazwa kwa uhuru wa Biafra on Tuesday Jumanne
Watoto wakitazama bango la picha mwezi tarehe 30, Mei 2017 mjini Abidjan, wakati wa maadhimisho ya 50 ya vita vya kiraia vya Nigeria . Nigeria iliadhimisha miaka 50 tangu kutangazwa kwa uhuru wa Biafra kuliko itumbukiza nchi hiyo katika limbo la vita vya wenyewe kwa wenyewe,huku kukiwa na hali ya wasi wasi na miito mipya ya kujitenga kwa jimbo hilo. Makundi makuu yanayounga mkono kujitenga jamii ya wazawa asilia wa Biafra (IPOB), na vugu vugu linalodai kutambuliwa kwa Biafra kama jimbo huru (MASSOB) - wameitisha siku ya kutafakari suala hilo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watoto hawa mjini bidjan, Ivory Coast, wanajifunza kuhusu vita vya wenyewe kwa njia ngumu sana - ya picha za wakati huo
Kindi jipya la wasishana wa shule wa Chibok waliookolewa walipowasili kwa usaidizi wa ushauri nasaha katika kituo cha maendeleo ya wa wanawake mjini Abuja . wazir wa masuala ya wanawake nchini humo alisema wasichana hao 82 wa kundi jipya lililookolewa watapelekwa tena shuleni mwezi Septemba kukamilisha masomo , lakini akasema hawatarudishwa kwenye shule yao ya awali

Chanzo cha picha, AFP/PGDBA ^ HND

Maelezo ya picha, Wasichana wa Chibok waliookolewa kutoka mikononi mwa wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram walianza kusaidiwa kurejea katika maisha ya kawaida katika mji mkuu wa Nigeria Abuja wiki hii
Ijumaa mchezaji wa soka wa Guinea Salif Sylla (kushoto) akiwa uwanjani wakati wa mchuoano wa kombe la dunia la vijana walio chini ya umri wa miaka 20 World Cup katika mchezo baina ya Guinea na Korea Kusini huko Argentina

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency

Maelezo ya picha, Ijumaa mchezaji wa soka wa Guinea Salif Sylla akiwa uwanjani wakati wa mchuoano wa kombe la dunia la vijana walio chini ya umri wa miaka 20 World Cup katika mchezo baina ya Guinea na Korea Kusini huko Argentina
MMoja wa wanamuziki wa bendi ya Ivory Coast "Magic System" inayojumuisha mwanamuziki A"Salfo (Kulia), akikutana na wanafunzi wa shule

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jumatanu, mwanamuziki maarufu wa Ivory Coast bendi Magic System alipotembelea shule yenye jina la bendi hiyo mjini Abidjan.
Wachezaji ngoma ya kitamaduni wakiwa wa Kongo wakipiga picha kabala ya kuonyesha onyesho lao nchini India

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wachezaji ngoma wa kikundi cha kitamaduni cha Wakongo walionyesha ngoma ya taifa la DRC mjini Bhopal, India, India siku hiyo .