Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa Picha: Treni yenye starehe na ghali yaundwa Japan
Treni ya Suite Shiki-shima imeundwa kuwapa abiria starehe lakini utahitaji kulipia gharama ya kati ya dola 2,860 na 10,000 na unaweza kuchagua kati ya safari ya siku mbili au nne.
Treni ya Shiki-shima ilifanya safari yake ya kwanza tarehe mosi Mei. Ilijengwa kulingana na mipango na michoro ya Ken Kiyoyuki Okuyama
Mandhari ya treni hiyo hukuwezesha kutulia huku ukifuhia glasi ya mvinyo
Treni hii ina nafasi kwa abiria 34 kwa hivyo ina nafasi ya kutosha abiria kuweza kuona vizuri
Hapa ndipo inaweza kulala baada ya safari ndefu
Mipango ya treni hiyo ilitangazwa na kampuni ya East Japan Railway Company mwaka 2014.
Chakula kitakuwa kikibakuliwa sehemu kama hii
Kila kitu kitakuwa sawa na cha hoteli yoyote ya kifahari
Unaweza pia kukaa karibu na moto