Papa Francis ataka mazungumzo kuhusu kusuluhisha mzozo wa Korea Kaskazini

Papa amesema mzozo baina ya mataifa hayo huenda ukazua vita vitakavyoangamiza watu wengi

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Papa amesema mzozo baina ya mataifa hayo huenda ukazua vita vitakavyoangamiza watu wengi

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis anataka mazungumzo ya kimataifa yafanyike kusuluhisha mvutano unaozidi kutokota kati ya Marekani na Korea Kaskazini akisema kwamba swala hilo limekuwa kaa la moto.

Papa Francis amewaambia wanahabari kwamba mzozo baina ya mataifa hayo huenda ukazua vita vitakavyoangamiza watu wengi.

Amesema kwamba umoja wa mataifa umepoteza nguvu zake.

Awali manowari ya kivita ya Marekani iliwasili karibu na rasi ya Korea, saa chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la kombora ambalo lilitibuka.

Korea Kaskazini imefanya majariio kadha ya makombora

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Korea Kaskazini imefanya majariio kadha ya makombora

Rais wa Marekani Donald Trump ameishutumua Korea Kaskazini kwa kuiokosea heshima jirani wake China na rais wake.

Hivi majuzi Trump alimulika rais wa China Xi Jinping na kumpongeza kwa kujitahidi kutatua mzozo wa Korea Kaskazini.

Jaribo la kombora la Korea Kaskazini lilijiri saa chache baada ya baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa kujadili mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini

Meli za Marekani zimewasili rasi ya Korea
Maelezo ya picha, Meli za Marekani zimewasili rasi ya Korea