Korea Kaskazini yasema itazamisha meli ya Marekani

USS Carl Vinson

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Meli ya USS Carl Vinson

Korea Kaskazini iko tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea, kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.

Taarifa katika gazeti la Rodong Sinmun lilisema kuwa meli ya Marekani ya USS Carl Vinson itazamishw kwa shambulizi moja.

Kundi la meli za Marekani zikiongozwa na Vinson zinatarajiwa kuwasili katika rasi ya Korea wiki hii.

Meli hizo zilitumwa na Rais Donald Trump baada ya onyo kuhusu uvumilivu kumalizika dhidi ya mpamgo ya nuklia ya Korea Kasakazini.

"Vikosi vyetu viko tayari kuzamisha meli hiyo ya kubeba ndege ya Marekani kwa shambulizi moja, lilisema gazeti la Rodong Sinmum.

USS Carl Vinson (kushoto) na meli zingine za vita zilikuwa bahari ya Hindi mwishoni mwa wiki

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, USS Carl Vinson (kushoto) na meli zingine za vita zilikuwa bahari ya Hindi mwishoni mwa wiki
Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
Maelezo ya picha, Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini