Ufaransa yamchagua rais mpya

Police officers patrol in Paris

Chanzo cha picha, AFP / Getty Images

Maelezo ya picha, Karibu polisi 50,000 na wanajeshi 7,000 wametumwa kote nchini

Raia wa Ufaransa wanapiga kura ya urais hivi leo.

Kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa , huu umekuwa uchaguzi usiotabirika.

Takriban asilimia 30 ya wapiga kura wanaaminika kwamba hawajatangaza msimamo wao.

Wawaniaji watatu wakuu hawana historia yoyote ya kisiasa akiwemo Emmanuel Macron, Marine le Pen na Jean-Luc Melenchon

Mpinzani wao mhafidhina Francois Fillon, amehudumia serikali katika nyadhfa kadhaa za uwaziri katika kipindi cha miongo miwili.

From L to R: François Fillon, Benoît Hamon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron and Jean-Luc Mélenchon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wagombea maarufu (Kushoto kuenda kulia): François Fillon, Benoît Hamon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron na Jean-Luc Mélenchon

Hakuna yeyote anayetarajiwa kuibuka na ushindi katika duru ya kwanza, na wawili watakaoongoza uchaguzi huo watamenyana na katika duru ya pili mwezi ujao.

Usalama umeimarishwa kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea katikati mwa mji mkuu Paris alhamis, ambapo afisa mmoja wa polisi aliuwawa.

A woman votes at the French consulate in New York

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baadhi ya wapiga kura walio nchi za nje tayari wamepiga kura zao