Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanafunzi wakwaruzana vikali na polisi Chile
Wanafunzi waliokuwa wakiandamana nchini Chile kupinga mabadiliko ya elimu wamekwaruzana vikali na vikosi vya usalama.
Mwezi machi katika mji mkuu Santiago, wanafunzi walirusha mawe kwa vikosi vya polisi ambavyo vilikuwa vikitumia gesi ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.
Maandamano kama hayo pia yamefanyika katika miji mingine miwili.
Rais wa Chile Michelle Bachelet ameamuru kuongeza idadi ya wanafunzi watakaopokea mkopo kwa elimu ya juu hii ikiendana na ukuaji wa uchumi.
Lakini wanafunzi wanataka kupata mkopo wa kusoma masomo ya ziada.