Kijana tajiri anayekwepa sheria Thailand

Kwa zaidi ya miaka minne Vorayuth Yoovidhaya hajafika mahakamani

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Kwa zaidi ya miaka minne Vorayuth Yoovidhaya hajafika mahakamani

Vorayuth Yoovidhaya, mjukuu wa billionea aliyeanzisha kinywaji cha Red Bull, huenda tena asifike katika mahakama ya Bangkok kujibu mashtaka yanayohusu kifo cha afisa wa polisi.

Tarehe 3 Septemba mwaka 2012, afisa huyo wa polisi aligongwa na gari la kifahari aina ya Ferrari lilokuwa likiendeshwa na bwana Vorayuth.

Majaribio kadha ya utawala wa Thailand kumfikisha Vorayuth mbele ya sheria, yanaonekana kuwa mvutano na familia tajiri nchini humo.

Ukweli kuhusu kuuawa kwa polisi uko wazi.

Ferrari iliyokuwa imeharibiwa vibaya ilipatikana kwenyejumba la familia

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ferrari iliyokuwa imeharibiwa vibaya ilipatikana kwenyejumba la familia

Polisi Wichian Klanprasert alikuwa akiendesha pikipiki yake mjini Bangkok, wakati aligongwa na gari aina ya Ferrari, ambayo iliuvuta mwili wake umbali wa zaidi ya mita 100 barabarani.

Maafisa wa kuchunguza waliyafuata matone ya mafuta ya breki hadi jumba la kifahari la familia hiyo tajiri lililo umbali ya kilomita moja hivi.

Gari hilo la Ferrari lililokuwa limeharibiwa vibaya, lilikuwa hapo na polisi wamamkama dereva aliyekuwa ameajiriwa na familia kama mshukiwa mkuu.

Red Bull ni wathamini wa Formula One

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Red Bull ni wathamini wa Formula One

Wakati polisi waligundua kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na bwana Vorayuth, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 27, alifanyiwa uchunguzi na kupatikana akiwa na kiwango kikubwa cha pombe kwenye damu

Tangua mwaka 2013 bwana Vorayuth amekataa kufika mara saba mbele ya mahakama, huku mawakili wakitoa sababu kadha zikiwemo kuwa yuko ziara za kibiashara nje ya nchi au anaumwa.

Lakini picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa na marafiki zake, zanaonyesha kuwa mara kadha amekuwa nchini Thailand na pia yeye husafiri kote duniani kushiriki mashindano ya uendeshaji magari kwa kasi na kustarehe.

Familia ya Yoovidhya inaaminiwa kuwa na mali ya thamani ya dola bilioni 20

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Familia ya Yoovidhya inaaminiwa kuwa na mali ya thamani ya dola bilioni 20