SpaceX yafanikiwa kutumia roketi mara ya pili

Chanzo cha picha, SPACEX
Kampuni ya kuunda roketi za wanasayansi wa anga za juu ya SpaceX iliyo na makao yake huko Carlifonia, Marekania, imefanikiwa kurusha tena roketi yake kwa kutumia moja ya roketi zake aina ya Falcon 9.
Awamu ya kwanz ya roketi hiyo ambayo ilitumika tena miezi 11 iliyopita, ilitumiwa kutuma satellite ya mawasilano kuenda kwa mzingo wa dunia, kutoka kituo cha safari za anga za juu cha Kennedy Space Center.
Hiyo ni hatua kubwa wa kampuni ya SpaceX katika majaribio ya kutumia roketi mara ya pili.
Kwa kawaida rekoti hutupwa kwa sababu uharibiwa wakati wa zishatumika.
Kampuni hiyo ya SpaceX ina lengo za kuzikarabati na kuzitumia tena roketi ambazo tayari zishatumika kwa minajili ya kupunguza gharama.

Chanzo cha picha, SPACEX
Chombo kinachoibeba satelite kwa sasa kinaendelea na safari kabla ya kuitundika satelite ya mawasiliano ambayo itatoa huduma ya mawasiliano kwa nchi ya Brazil, nchini za Caribbean, Amerika ya kati na Amerika Kusini.
Kwa miaka miwili iliyopita SpaceX imekuwa ikirudisha sehemu za kwanza za roketi zake ardhini baada ya sehemu hizo kutimiza wajibu wa kuinua mzigo ulitundikwa juu yake.
Sehemu hizo za kwanza hurudi peke yao na kutua salama katika chombo kinachoelea baharini.
Sasa sehemu zingine za kwanza zilizorudi na kutua salama zitatumiwa tena kurusha roketi zingine mwaka huu.

Chanzo cha picha, SPACEX

Chanzo cha picha, AIRBUS DS












