Hong Kong yamchagua kiongozi mpya wa kwanza mwanamke

Chanzo cha picha, Reuters
Carrie Lam amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa Hong Kong, akiwa ndiye mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.
Bi Lam mwenye umri wa miaka 59 aliungwa mkono na serikali ya China na alitarajiwa sana kushinda,
Hong Kong ina uhuru kutoka China lakini maandano yamekuwa yakiongezeka kupinga uingiliajia wa China.
Kiongozi wa Hong Kong hachaguliwi na wananchi bali kamati ya watu 1200 iliyo na watu wengi wanaoipendelea China.
Makundi ya kupigania demokrasia yamekuwa yakifanya maandamano nje ya eno kulikofanyika uchaguzi huo na kuutaja kuwa usio wa haki.

Chanzo cha picha, EPA
Mshindani mkuu wa Bi Lam ambaye ni mkuu wa zamani wa masuala ya uchumi John Tsang, alikuwa akipendelewa na watu kwa mujibu wa kura ya maoni.
Mgombea wa tatu alikuwa ni jaji mstaafu Woo Kwok-hing.
Bi Lam alipata kura 777 huku Tsang akipata kura 365 na Woo kura 21.
Wito wa kufanyika kwa uchaguzi huru umeshindwa licha ya kushuhudiwa maandamano makubwa.
Kamati ya uchaguzi mjini Hong Kong ilimchagua Bi Lam kuchukua mahala pa kiongozi wa sasa CY Leung, ambaye ataondoka madarakani mwezi Julai.












