China yajisifu kwa kuwafunga wanaotetea haki za binadamu

Chanzo cha picha, Getty Images
Mahakama kuu nchini Uchina, imesema kuwa mojawepo ya hatua zake kuu mwaka jana, ni kuwafunga jela wanaharakati wa kutetea haki za binadamu.
Katika ripoti iliyowasilishwa bungeni na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Zhou Qiang, alijisifia hukumu kali waliyopewa wale wanaoaminika kuhujumu usalama wa taifa.
Wakili na mwanaharakati, Zhou Shifeng, ni miongoni mwa wale ambao utawala nchini humo unajisifia kuwafunga jela.

Chanzo cha picha, AP
Alihukumiwa jela miaka saba hapo mwezi Agosti mwaka jana, kwa kudharau mamlaka ya nchi hiyo.
Shirika la Amnesty International, linasema kuwa hukumu dhidi ya wanaharakati imechochewa kisiasa.

Chanzo cha picha, Getty Images








