Ivanka Trump kupewa ofisi White House

Chanzo cha picha, AFP
Binti yake rais wa Marekani Donald Trump, Ivanka, atapewa ofisi kwenye ikulu ya White House, kwa mujibu wa afisa mmoja.
Lakini hata hatakuwa na cheo chote wala kulipwa mshahara wakati akifanya kazi upande wa West Wing.
Afisa huyo alithibitisha ripoti za vyombo vya habari kuwa Ivanka, mwenye umri wa miaka 35, atakuwa na uwezo wa kupata taarifa za siri.
Wajibu wake utakuwa ni kama "macho na maskio" ya Trump, huku akitoa ushauri tofautia, kwa mujbu wa wakili wake.

Chanzo cha picha, EPA
Ivanka ambaye ana kampuni ya mitindo, ataujiunga na mumewe Jared Kushner, ambaye ni mshauri wa rais.
Ushawishi wa wawili hao kwa rais Trumo imeibua maswali mengi.
Pia ushawishi huo umezua mjadala ikiwa kuna mipaka kati ya shughuli za kisiasa za Trump na zile za kibiashara.
Tangu kuapishwa kwa Trump mwezi Januari, Ivanka ameonekana akihudhuria mikutano na viongozi wa dunia, akiwemo waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Chanzo cha picha, Reuters

















