Wenger ni mbinafsi amsema Sutton

Chanzo cha picha, Rex Features
Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Chelsea ya England, Chris Sutton, amesema kocha wa Arsenal Arsene Wenger ni mbinafsi kwa kuwa anaendelea kuwa kimya juu mustakabali wake wa kuendelea kuinoa Arsenal
Akizungumza na BBC Radio5 Sutton amesema Wenger ni kama Mjomba anayengangania kutokutoka katika tafrija. Na amekua akiirudisha timu nyuma siku zinavyozidi kwenda.
"Amekua akifeli katika nyakati za soko la usajili, fanya jambo sahihi kama huwezi tuambie huwezi ." ameeleza mchezaji huyo.

Chanzo cha picha, Google
Wenger alianza kunioa klabu ya Arsenal toka 1996, na mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa ligi kuu ilikua ni mwaka 2004 na sasa timu inashika nafasi ya sita katika msimamo ligi.








