Simu ya Adolf Hitler kupigwa mnada Marekani

Simu iliokuwa ikitumiwa na kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler kupigwa mnada Marekani

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Simu iliokuwa ikitumiwa na kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler kupigwa mnada Marekani

Simu iliyokuwa ikitumiwa na Adolf Hitler wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia itapigwa mnada nchini Marekani mwisho mwa juma hili.

Simu hiyo nyekundu iliyo na chapa cha jina la kiongozi huyo wa Wanazi, ilipatikana katika ngome ya Hitler jijini Berlin mwaka 1945.

Wanajeshi wa Urusi walimpa mwanajeshi wa Uingereza, Brigedia Sir Ralph Rayner, kama kito cha kumbukumbu, muda mfupi baada ya Ujerumani kukubali kushindwa katika vita hivyo.

Simu ya Adolf Hitler

Chanzo cha picha, AFP/Getty images

Maelezo ya picha, Simu ya Adolf Hitler

Kampuni hiyo ya mnada iliyoko Maryland, ilisema kuwa shughuli za mnada zitaanza kwa bei ya Dola 100,000.