''Tuzo za Grammy hazina ubaguzi''

Chanzo cha picha, Getty Images/BBC
Msanii Adele alishtuka wakati alipomshinda Beyonce katika orodha ya albamu bora katika tuzo za Grammy.
''Siwezi kukubali tuzo hii'' ,alisema alipoivunja {kwa bahati mbaya} tuzo hiyo.
Hatahivyo aliikubali tuzo hiyo baadaye licha ya kupinga kwamba Beyonce alifaa kushinda .
Lakini swala hilo lilizua madai kwamba tuzo za Grammy zina ubaguzi, hususan kwa kuwapuuza wasanii weusi na kuwapendelea wasanii weupe ambao inawapigia upatu.
Katika kipindi cha miaka 10 iliopita ni msanii mmoja mweusi pekee aliyeshinda tuzo hiyo baada ya kujishindia albamu bora ya mwaka: Herbie Hancock ambaye albamu yake 2008 River iliojumuisha nyimbo za Joni Mitchell.








