Iran yawaruhusu wamarekani kuingia nchini mwake

Kiongozi mkuu wa Iran Khamenei (kushoto) na Rais Rouhani (kulia)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi mkuu wa Iran Khamenei (kushoto) na Rais Rouhani (kulia)

Iran imetangaza kukubalia kikosi cha wanamieleka wa Marekani kushiriki mashindano ya dunia, yatakayofanyika nchini humo baadaye mwezi huu.

Awali Iran walisema kuwa wamarekani hawatakubaliwa kushiriki mashindano hayo.

Walinyimwa visa, baada ya Iran kusema kwamba itawapiga marufuku raia wa Marekani kama jibu kwa marufuku ya Rais Donald Trump kwa wairan kuzuru Marekani.

Wizara ya nchi za kigeni mjini Tehran, imesema kwamba, uamuzi wake wa sasa wa kuwakubalia wanamieleka wa Marekani ni sehemu ya uamuzi wa mahakama nchini Marekani kuahirisha kwa muda amri hiyo kuu ya Trump.