Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Facebook yapata faida
Kampuni ya mtandao wa facebook imeripoti kuongezeka kwa faida katika ripoti yake ya robo ya kwanza ya mwaka 2016.
Kampuni hiyo ilijipatia zaidi ya dola bilioni tatu na nusu ,na kupita makadirio .
Hisa zake zilipanda thamani kwa asilimia 2 baada ya biashara ya saa moja.
Kwengineko mahakama moja ya kijimbo nchini Marekani imeitaka facebookm kuilipa dola milioni mia tano kampuni ya uchapishaji wa videogame ZeniMaxMedia kwa kutumia kodi ya kumpyuta yake ili kuzindua Virtual Reality Headset.
ZeniMax ilidai kwamba mfanyikazi wake mmoja wa zamani ambaye sasa ndio afisa mkuu wa maswala ya teknolojia katika facebook alianzisha teknolojia hiyo wakati bado alipokuwa akiifanyia kazi kampuni hiyo.